Bukobawadau

BENKI YA DUNIA YATOA FEDHA KUJENGA MIRADI YA MAJI BIHARAMULO

 1 Mhandisi wa maji katika Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Bw Davidi Kaijage (katikati )na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Apolinari Mugarula wakiwa na kanali  Fabian Massawe wakieleza ujenzi wa tanki la maji katika kata ya Nyakahura unaofadhiliwa  na Benki ya dunia kiasi cha Tsh Bil 1. 444
 Tanki la  maji litakalokuwa na  ujazo wa lita 90,000
 Chanzo cha Maji  
 wananchi na mkuu wa mkoa wakichunguza utando mwekundu wa magugu majikwenye chanzo hicho.
 Waliokaa meza kuu  kushoto ni mkuu wa wilaya ya Biharamulo Richard Mbeho na kulia ni mwenyekiti wa halmashauri Apolinari Mugarula
Mhandisi akitoa taarifa ya mradi wa maji kwa mkuu wa mkoa
Mkuu wa mkoa akiongea na wazee wa kata ya Nyakahura Biharamulo wakishukuru serikali kuwapatia huduma ya Maji

Jumla ya shilingi Bil 1.444 zimetolewa na benki ya dunia kujenga mradi wa maji katika kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo ili kusaidia wananchi kuepukana na kukosa huduma hiyo ambayo walikuwa wakiitafuta kwa kutembea umbali mrefu
Mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Bw Davidi Kaijage amesema  December 23  mwaka huu wakati akitoa taarifa ya fedha na matumizi yake kwa mkuu wa mkoa wa kagera kanali mstaafu Fabian Masawe alipotembelea mradi huo  ili kujiridhisha na hatua za ujenzi unaoendelea
Bw Kaijage amesema  Chanzo cha maji cha Mabare kitasambaza maji katika vijiji vinne vya Mabare Nyantakara Mihongora na Nyakahura  ambapo wakazi 24 332  walioko katika kaya 3804 watapata huduma ya maji zikiwemo taasisi mbalimbali kwenye vijiji hivyo
Mhandisi huyo amesema kuwa  mradi huo  utahudumia shule za msingi na sekondari  Nyakahura , shule ya msingi Gwasero na Mihongora  kituo cha Afya Nyakahura ,Zahanati ya Ngararambe machinjio na masoko yaliyoko vijijini.
“Tanki la maji lina ujazo wa lita  90,000 usambazaji mabomba  mita 19,838 nakuna vituo vya kuchotea maji 46 kumechimbwa mitaro mita 30,345”.Alisema Kaijage
Ameongeza kuwa ujenzi wa visima na vituo vya maji  unafanywa na FEMA Builders LTD  na malipo yaliyokwisha fanyika ni 606,176 000 pia mkandarasi mshauri kalipwa 36,447000 ambapo hadi kufikia 21 Desemba ni jumla ya malipo ya Tsh.64,265 3000
Kwa upande wake  diwani wa kata ya Nyakahura ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Bw Apolinari Mugarula amesema kuwa taasisi zitakazonufaika zaidi ni kituo cha afya pamoja na shue ya sekondari Nyakahura zikiwemo na shule za misingi katani humoAmesema kuwa wananchi kabla ya kuanzishwa mradi huo walikuwa wakiteka maji kwenye madimbwi ambapo walilazimika kufukuzana na mifugo huku maji hayo yakiwa sio safi wala salama kiafya  jambo ambalo liliwafanya wananchi wakiwemo watoto kuwa na homa ya matumbo kutokana na minyoo ya mani machafu
 Hata hivyo mkuu wa mkoa wa kagera kanali Masawe amewataka wananchi wa vijiji hivyo kutunza na kuhifadhi mradi huo utakaokuwa na manufaa katika shughuli za kuwaletea maendeleo na kupunguza mateso ya wanawake na watoto wa kike na wazee kutafuta huduma hiyo sehemu za mbali.
Na shaaban Ndyamukama
Next Post Previous Post
Bukobawadau