KIGOGO WA CCM WILAYANI NGARA AHAMIA CHADEMA
Dk Peter Bujari. Picha kutoka Maktaba
NA Shaaban Ndyamukama December 27, 2013
Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Ngara mkoani Kagera ambaye aliwahi kugombea nafasi ya ubunge mwaka 2010 kupitia chama hicho Dr Peter Bujali amekihama chama chake na kutangaza kujiunga na chadema wilayani humo
Uamuzi huo ameutoa jana kwa waandishi wa habari na kwamba ameamua kujiondoa ndani ya ccm kwa kuwa hakuridhika na utendaji kazi wa serikali inayoongozwa na chama hicho na kuwafanya wananchi kuendelea kukosa maendeleo kwenye mazingira yanayowazunguka
Dr Bujari amesema serikali imejenga matabaka kati ya matajiri na maskini na kuwafanya wananchi walio na kipato duni kiuchumi kuathirika na mfumo tawala wa ccm ambao watoto wa maskini wanachaguliwa kwenda katika kusomea kwenye shule za kata ambazo hazina miundombinu
Alisema kuwa katika sekta hiyo ya elimu mfumo umekuwa wa kuwapeleka wanafunzi ambao wazazi wao wana fedha zaidi shule za private na maskini wanakosa taaluma bora kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha nne
“Ngazi hizi wanafunzi wanhitaji kujengewa misingi ya kuwa wanasayansi na viogozi wakuongoza taifa hili kwa kuwa walioko kwenye nafasi umri wao unachechemea lakini wanafisadi nafasi na mising ya utawala bora”.Alisema Dr Bijari.
Aidha amesema serikali na chama tawala viongozi wake wameshindwa kuwajibisha wanaouza madawa ya kulevya na kuhujumu uchumiwa taifa na kulifanya Taifa la Tanzania kukosa thamai mbele ya mataifa mengine na kuwafanya hata wasomo walioko kwenye mataifa hayo kutoaminika
Alidai kuwa chama tawala katika ilani yake iliahidi kutatua kero ya maji na Afya lakini wananchi wanazidi kutaabika kwa kukosa huduma hiyo licha ya ilani kutangaza changamoto hizo kukoma ifikapo mwaka 2014/2015.
Aliongeza “Desemba 28 2013 (kesho ) nakabidhiwa kadi ya chadema wilayani Ngara na nitaendelea na harakati zangu za kutetea haki za binadamu kwa kupata huduma bor za afya elimu na maji na hii ni kutaka kuleta mabadiliko kwa kushirikiana na wafuasi wake ”
Naye mbunge mstaafu wa jimbo la Ngara ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani kagera Bw Pius Ngeze amesema kuwa hana maoni juu ya kuhama kwa mwanachama huyo ambaye alikuwa naye kwa ukaribu katika kuhamasisisha wananchi wilayani Ngara katika kupambana kuondoa umaskini.
Hata hivyo siku chache Ngeze akiongea na mwandishi wa gaeti hili alisema wananchi hawana imani na serikali na chama tawala kwa kuwa wanaopewa nafasi hawawajibiki kama inavyotakiwa na hivyo kusababisha wanachama kukimbilia vyama vingine.
Alisema kuwa baadhi yao wanfanya kazi kwa mazoea na sio waaminifu katika nafasi walizopewa ama kwa kuchaguliwa au kuteuliwa na hivi sasa wao ndio vinara wa hujuma kwa kukaa maofisini bila kutembelea jamii kuelimisha juu ya utaalamu wa kazi zao.
Dr Bujali alijiunga na ccm mwaka 1995 na amekuwa akijuhusisha na utoaji wa huduma za kijamii hasa elimu na afya katika wilaya ya Ngara kupitia shirika lake la HUMAN DEVELOPMENT TRUST (HDT) ambapo amesaidia kuhamasisha jamii kuondokana na magonjwa ya malaria na kusaidia jamii zenye uwezo duni
Pamoja na jitihada zake ametoa msaada kwa watoto yatima kuwaendeleza kielimu katika wilaya za Ngara na Biharamulo huku baadhi ya familia zikipewa mitaji ya fedha ama mifugo (mbuzi kuendeleza maisha nankuongeza kipato cha familia.
Mwaka 2010 alikuwa kwenye orodha ya wanachama 10 wa CCM waliowania nafasi ya ubunge kwenye jimbo la uchaguzi la Ngara ambapo wanachama walimpa kura 2713 na aliyepata nafasi hiyo ni mbunge wa sasa kupitia chama hicho Deogratias Ntukamazina aliyepata kura 4900 za wanachama wa CCM.
MWISHO
MWISHO