Bukobawadau

LEO TENA KUTOKA KURASA ZA WADAU MBALIMBALI 4 DEC,2013

Willy Kirouera Rutta:
Nisaidieni jamani kwa kutoa maoni yako- Hivi kwanini vijana wengi ambao ni wahaya HAWAPENDI KUJITATAMBULISHA KUWA NI WAHAYA, wanapenda kuona fahari ya kujitambulisha kuwa mi sio mhaya kwani sikuzaliwa Bukoba, wengine Mama mchaga, utasikia sikusomea wala sijui kihaya, wengine mi mhaya wa kiharabu, WENGINE BIBI MZAA BABA NDIO MHAYA. Mimi binafsi ni mhaya origanal na naona fahari kujitambulisha - We unasemaje kwa mtu anayekataa uasili wake? toa maoni yako
Mdau Rama. S. Msangi; Picha hii ya othman Michuzi, inamuonyesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Bilal (kulia) akibadilishana mawili matatu na Ole Njolay, ambaye ni balozi mpya wa Tanzania nchini Nigeria, muda mfupi kabla ya makamu wa rais kumuaga mhe. Njolay ambaye anakwenda huko kuanza majukumu yake ya uwakilishi wa nchi.

Hivi mzee Njolay alikuwa wapi vile maana hapa kati sijamsikia sikia aisee. Halafu, hatuna damu changa ambazo zingeweza kufanya majukumu kama haya ya kibalozi kwa kutumia busara za wazee wetu hawa, hadi wenyewe waendelee kuwa mstari wa mbele?
Dunstan Mutagahywa  
KWA NINI TANZANIA KUPITIA KAGERA INA KILA SABABU YA KUIOMBEA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI MAISHA MAREFU? 
Najiuliza kama Tanzania imeishatambua kuwa Mkoa wa Kagera ndiyo sehemu ambayo haswa nchi inaweza kuitumia kuwekeza ili ifaidike na jumuiya ya Afrika Mashariki! Mf. Kagera inapakana na nchi zote za AAfrika Mashariki ispokuwa Kenya tu, lakini hata kama Sudan Kusini au Congo zingeruhusiwa baadae kujiunga, bado Kagera ingekuwa kama Kitovu! Sasa najiuliza wakubwa wetu hili hawlioni kwamba ,kw mfano wanaweza kujenga uwanja mkubwa wa ndege tuseme maeneo ya omukajunguti kule Kyaka, je hiyo reli wanayoisema Museveni, Kagame na Kenyata h, sisi Tanzania htuwezi tukaiunganisha nasi ikatokea Kampala ikatokea Karagwe/Kyerwa mpaka - Benako/Ngara hadi Rusumo mpaka wa Rwanda na Tanzania? na ikatoka benako mpaka mpaka wa Burundi/Bujumbura na kutoka Benako ikaunganishwa mpaka kule Isaka Kahama ikakutana na reli yetu ya Kati, au hata ikiletwa mpaka maeneo ya Kyaka ikitokea Kampala -mutukula,likajengwa bandari ya nchi kavu pael ili mizigo ikawa inaletwa kwa malori hadi Bandari ya Bukoba na Kemondo ambazo zinaweza kuboreshwa, sambamba na zile za Mwanza na Musoma? Vile vile watu wa mkoa wa Kagera wana mahusiano ya muda mrefu na watu wa mataifa haya ya Burundi,Rwnda na Uganda,kwa hyo uhusiano huu unaweza kutumika kurahisisha mahusiano zaidi ya hasa kiuchumi kwa upande wa Tz! Tusilale, tusiingie kwenye jumuiya kama fashion, wenzetu wa nchi jirani kuna kitu wamenyemelea kwetu sisi je? Ukienda Ngara kuna bidhaa nyingi za Rwanda na Burundi mf vitenge, ukienda Karagwe na Misenyi ,Muleba na hata Karagwe hapo ndo usiseme ni bidhaa za Uganda kwenda mbele! Yaani wahaya husema " Zigwa mbali batazilya" Jumuiya ya Afrika Mashariki ni km Zawadi kwa wa Tz kupitia mkoa wa Kagera au?
Na Dunstan - Diwani Kata Kamachumu.
 Matukio ya  kitchen party ya mwanadada Rachel harusi yake itafanyi siku ya jumamosi
Picha na Mdau Saraha Katarama
Wanasema "appointee is appointed under the discretion of the appointer"
Salim Kikeke.
MAFANIKIO hayawezi kutokea bila juhudi na kujinyima. Ili ufanikiwe unatakiwa kujinyima vitu vizuri ambavyo nafsi yako inatamani sasa kwa muda fulani ili baadaye uishi kwa furaha na kuipa nafsi yako vyote inavyovihitaji. Kanuni sahihi ya kufikia hilo ni kutumia asilimia 30 ya unachokipata na kuhifadhi 70. Hii ni kanuni ngumu lakini iliyowafanikisha wengi walio na mafanikio makubwa sasa. -Joseph Shaluwa
Mubelwa Bandio 
Mdau Mubelwa Bandio;Kauli yangu ilikuwa...
HUU WARAKA UTALETA NYARAKA NA MAELEZO MENGI TOKA KWA WENGI WENYE USHAWIKI KWA WENGI.
Nilisema..
MAAMUZI YA CC YALITATUA HOFU YA VIONGOZI LAKINI HAYAKUTOA WALA KUJIBU DUKUDUKU LA "MWANANCHI MIMI"
Nilisema.....
BAADA YA "HYPER" ZA WARAKA KUPOA, WATU WATATAKARI NA MENGI YATAUNGWA MKONO.
"If you think the judgement started, there's so much more left to come..." Morgan Heritage


JIUNGE NA UKURASA WETU MPYA WA FACEBOOK KUPITIA HAPA https://www.facebook.com/Bukobawadau?ref=hl
KAPOTIVE Star Singers-BUKOBA singers. From Left to Right.
Denis Deus (Public relations officer), Edina Kilama (singer), Claudius Mutabuzi(Treasurer), Thersia Kagya (Secretary), Alexander Ndibalema(Director) and Editha (singer).

Please don't forget to visit our facebook page and "LIKE" it. Also see some of our songs onwww.youtube.com/USER/KAPOTIVE.
.
Mh. Peter  Msigwa.
Mkakati mkubwa umeandaliwa wa na BAADHI ya vyombo vya habari ,wa kuwachafua BAADHI ya wabunge na viongozi wa chadema nikiwemo na Mimi, kwa kuandika habari za UONGO na kutunga,,BAADHI ya magazieti hayo ni habari Leo na jambo Leo .binafsi hainikatishi Tamaa .zaidi sana inanifanya nigundue kuwa nafanya kazi sahihi ya wananchi. 
 Wadau wakifurahi na Windhoek Lager ndani ya East 24 Bar& Grill.
Mdau Jerome  Rugemalira

JIUNGE NA UKURASA WETU MPYA WA FACEBOOK KUPITIA HAPA https://www.facebook.com/Bukobawadau?ref=hl
Next Post Previous Post
Bukobawadau