Bukobawadau

OFISI YA WAZIRI MKUU YAZINDUA MRADI WA KUIJENGEA JAMII UWEZO WA KUPUNGUZA ATHARI ZA MAAFA KWA MIKOA ILIYOATHIRIKA ZAIDI NA UKAME

Mratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa Iliyoathirika Zaidi Na Ukame Bw. Harrison Chinyuka akifafanua jinsi Mradi huo utakavyotekelezwa katika Wilaya za mikoa ya Kilimanjaro na Shinyanga, Mradi huo umezinduliwa leo  Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro,  (kulia mwenye suti) ni Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia maelezo ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa Iliyoathirika Zaidi Na Ukame ambao kauli mbiu yake ni; Athari Za Ukame, Zinapunguzika Jamii Husika Ikijengewa Uwezo, (wakwanza kushoto ) ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Same ASP. Ally Mhalule, mradi huo umezinduliwa leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Same (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi akisisitiza jambo juu ya Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa Iliyoathirika Zaidi Na Ukame wakati wa Uzinduzi wa Mradi huo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Same (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wajumbe kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi (katikati kwa walio kaa) mara baada ya uzinduzi wa Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa Iliyoathirika Zaidi Na Ukame ambao kauli mbiu yake ni; Athari Za Ukame, Zinapunguzika Jamii Husika Ikijengewa Uwezo, mradi huo umezinduliwa leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Same. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Next Post Previous Post
Bukobawadau