Bukobawadau

AJALI MBAYA MANYONI WATU 13 WAPOTEZA MAISHA PAPO HAPO

Ajali mbaya ya gari iliyotokea Wilayani Manyoni Mkoani Singida mapema leo asubuhi , gari aina ya NOAH na Lori aina ya Scania yamegongana Uso kwa uso na kupelekea Watu  13 waliokuwa ndani ya Noah kufariki DUNIA papo hapo,Mdau Shenyongo Mkazi Mutukula ni mmoja wa kati ya waliopoteza maisha katika ajali hii.
Hili ndilo Lori  liliogongana na Noah,eneo la Isuna Manyoni,Dereva na utingo wa Lori inasemekana wamekimbia  baada ya ajali hiyo kutokea pamoja na kuwa Utingo amevunjika mguu
Kwenye gari  kabaki Mbuzi tu!!!
Chanzo kinasema  gari aina ya NOAH ilikuwa imebeba abiria kutoka Itigi wakielekea Singida Mjini.
CREDIT;Mdau Mainda.


Next Post Previous Post
Bukobawadau