Bukobawadau

GAZETI LA CHAMPIONI LAPONGEZWA

Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (kulia) akimpa zawadi ya shilingi elfu hamsini (50,000) Bi. Rose Majembe baada ya kumkuta kwenye biashara yake ya kukaanga mihogo, Mwenge jijini Dar es Salaam. Katikati ni wahariri wa Championi, John Joseph na Philip Nkini mwingine ni dada aliyekutwa akinunua mihogo.
Mhariri Kiongozi wa Championi, akizungumza na msomaji wa gazeti hilo aliyemkuta maeneo ya Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally na wahariri wake John Joseph na Philip Nkini wakimpa zawadi ya chupa ya chai mwanamama huyu waliyemkuta maeneo ya Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam akisoma gazeti la Championi.
Bodi ya Uhariri ya Championi ikimpongeza askari wa JWTZ baada ya kumkuta akisoma gazeti la Championi.

BODI ya Uhariri ya Gazeti la Championi, leo ilitembelea maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wasomaji wake ambao walitoa maoni mbalimbali ambapo walilipongeza gazeti hilo kutokana na habari zake makini.

(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

Next Post Previous Post
Bukobawadau