Bukobawadau

KATIBU CCM JELA KWA UDANGANYOFU

KATIBU wa Itikadi Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kyerwa, Ferdinand Bishanga (38), amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia mali kwa udanganyifu.
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Karagwe na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Peter Matete, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Hakimu Matete alisema baada ya kumaliza kifungo, mshitakiwa atalazimika kulipa fedha hizo kwa mlalamikaji.
Alisema ametoa hukumu hiyo ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu pamoja na kuhitaji utajiri wa haraka.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Juma Lipwata, alieleza kuwa mshitakiwa alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Oktoba mwaka juzi.
Alidai mshitakiwa alipokea sh milioni 9 kwa udanganyifu kutoka kwa Vedasto Marchela, mkazi wa Kata ya Kayanga kwa lengo la kumnunulia kahawa kwa njia ya magendo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau