Bukobawadau

LEO KATIKA KUMBUKUMBU MWAKA 1997 KIKOSI CHA RTC KAGERA CHAIZUIA SIMBA KUTWAA UBINGWA.!!

Leo katika kumbukumbu na Bukobawadau Blog, Mwaka 1997 michuano ya ligi kuu tanzania bara ikiwa ukingoni kabisa ambapo mchezo wa mwisho ulifanyika Mjini hapa ndani ya uwanja wa kaitaba kati ya Simba Fc v/s RTC Kagera maarufu kama Wagadi, Simba ilihitaji ushindi ili ibebe kombe,lakini mambo yalienda ndivyo sivyo wakapokea kichapo cha mabao 3-1, kutoka kwa kikosi mahiri cha wachezaji wa RTC  Kagera.
Kumbukumbu zinaonyesha  wachezaji wa timu ya RTC waliokuwa wamekalia  benchi chini ya Kocha wao Mzee Sonday Kayuni kama/sub  ni Bure Mtagwa, Issa Ally, Zahoro Sabuu( check bob),marehemu Mukama Ntale,Patric Oswin,Mustapha Simba,Albert Sengo, mtu wa skendo kwa nyakati hizo Salmin Kamau na Endrew Kabaya.
Ushindi ulipatikana kupitia mikakati na mbinu pamoja na ushirikiano kati ya RPC wa Mkoa kipindi hicho  Marehemu Jumbe na Mkuu wa Mkoa aliyekuwepo Mzee Mangula.
Kikosi kamili uwanjani ni kama ifuatavyo.
 1.  ONESMO      EDWARD            
 2.  ABDUL        KITUMBA
 3.  JOHN            FAYA
 4. ABUU           OMARY
 5. GODWINI     KICHEMU 
 6. OMARY        SAID
 7. MOVISHA    HAULENA
 8. KASIGA       MACHAPATI
 9. CLEMENT   KAHABUKA
 10. FULGENCE NOVATUS  
 11. MUSSA  MASSARO  
Next Post Previous Post
Bukobawadau