MAMBO MUHIMU KUHUSU FACEBOOK IKIWA LEO FEB 4,2014 IMETIMIZA MIAKA 10
Leo February 4, mtandao wa Facebook unaadhimisha miaka 10 tangu ulipoanza kufanya kazi rasmi tarehe 4 February mwaka 2004 katika chumba kidogo cha bweni katika chuo kikuu cha Harvard kwa lengo la kuwaunganisha wanafunzi wa chuo hicho na marafiki zao.
Kwasasa mtandao wa Facebook una takriban watumiaji Bilioni 1.23 duniani kote. Licha ya kutumika katika mawasiliano, mtandao wa Facebook umefanikisha kupanua soko la bidhaa mbalimbali kwani kwa kutumia mtandao huu makampuni na watu binafsi wametangaza biashara na huduma zao kwa ufanisi wa hali ya juu, jambo hili limepelekea mtandao wa
Facebook kupata faida kubwa sana hasa kupitia matangazo ya Fan pages {Wapo walio nielewa na wengine najua bado hamjanipata any way, hebu tuendelee ntawaelekeza siku nyingine}, Kwa upande mwingine wapo walio lizwa na Facebook, wapo walio liza watu, wapo walio Fukuzwa kazi, Wapo walio pata kazi, Wapo wanafunzi walio feli kutokana na Facebook {Vilaza} pia wapo walio Faulu kwa kutumia vyema mtandao huu.
Mtandao wa Facebook unazidi kuboreshwa kila kukicha ili kutoa huduma bora kwa watumiaji na kustahimili ushindani wa wimbi la mitandao ya kijamii inayo ibuka kila kukicha.
Na Benchi la Teknolojia VIA Bukobawadau Blog