Bukobawadau

RATIBA YA SHUGHULI YA MAZISHI YA MAREHEMU MAMA THEONESTINA RWEYEMAMU HUKO NEW YORK

Ratiba fupi ya shughuli za msiba wa mama Theonestina Rweyemamu ni kama ifuatavyo:
  • Leo Jumatano tarehe 5 Februari 2014 kuanzia saa kumi jioni hadi saa mbili usiku ni kuaga Mwili wa Marehemu Mama Theonestina Rweyemamu. Mahala: Camelot Funeral Home, 174 Stevens Avenue, Mount Vernon, NY 10550;
  • Kesho Alhamisi tarehe 6 Februari 2014 saa nne asubuhi kutakuwa na Misa ya Kumwombea Marehemu kwenye kanisa la Moyo Mtakatifu au Sacred Heart Church. Mahala: 115 Sharpe Blvd., South Mount Vernon, NY 10550
  • Kusafirisha mwili wa Marehemu kwenda Tanzania inategemewa kuwa siku ya Ijumaa, tarehe 7 Februari 2014.
Watoto wa Marehemu kina Doris, Steven, Emmanuel na Diana pamoja na familia nzima wanapenda kuwashukuru wote kwa kufika kuombeleza nao na kwa rambirambi zenu. Wanapenda vile vile kuwashukuru WESTADI - NSSF.
Pamoja na ratiba iliyotajwa hapo juu, bado mnaweza kutuma rambirambi zenu kwao na kufika nyumbani kuwaona. Address ni: 40 East Sidney Avenue, Apt # 10C , Mount Vernon, NY 10550. Na namba ya simu ya nyumbani ni 914-667-6456.

Familia itashukuru kwa msaada wowote wa kuwasaidia kuweza kufanikisha mpango wa kumsafirisha mama Theonestina Rweyemamu kwa kutoa chochote kwenye Bank of America, account number 483044166145 routing number 021000322 na jina kwenye account ni Doris Rweyemamu. Familia vile vile inawashukuru wote waliojitolea mpaka sasa kufanikisha shughuli za msiba huu.

Kwa maelezo zaidi unaweza piga simu kwa wafuatao:

Emmanuel Rweyemamu 6462342418, Steven Rweyemamu 3028837971, Dr. Abbas Byabusha 9145847502, Doris Rweyemamu 6463799135.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Amen.

Uongozi-Jumuiya ya Watanzania New York.

MWISHO WA TANGAZO LA LEO FEB 5,2014

Taarifa Zaidi za Maendeleo ya Msiba wa Mama Theonestina Rweyemamu

Familia inahitaji kukusanya kiasi cha Dolla 10,000. Mpaka sasa kiasi cha Dolla 6,000 zimeshapatikana na kuna mapungufu ya dola 4,000.
 
Uongozi wa Jumuiya unawaomba Wanajumuiya kujitolea ili kufikisha kiasi cha fedha kinachotakiwa. Na kwa vile mipango ya kumsafirisha mama Theonestina Rweyemamu ni kati ya Ijumaa na Jumamosi ya wiki hii. Tunawaomba wanajumuiya tujitolee ili tuweze kufanikisha shughuli hizi. Kwa Wanajumuiya wa Queens na Brooklyn Mweka Hazina Msaidizi Dr. Temba atakusanya michango na kuiwakilisha kwa Familia ya Marehemu (na simu yake ni 646-489-6532) na kwa wanajumuiya wengine tunaomba mwasiliane na familia moja kwa moja au kwa kupitia Emmanuel Rweyemamu 6462342418, Steven Rweyemamu 3028837971, Dr. Abbas Byabusha 9145847502, Doris Rweyemamu 6463799135. Tunawaomba Watanzania wote tusaidiane katika kuhakikisha mipango yote kama ilivyotajwa hapo juu na ilivyotajwa kwenye email iliyopita inafanikiwa.
 
Kwa wale wanaotaka kutuma michango kupitia Benki, Familia itashukuru msaada wowote wa kuwasaidia kuweza kufanikisha mpango wa kumsafirisha mama Theonestina Rweyemamu kwa kutoa chochote kwenye Bank of America, account number 483044166145 routing number 021000322 na jina kwenye account ni Doris Rweyemamu. 
 
Tunaomba kuwakumbushia Watanzania wote na Wanajumuiya kuzisoma emails zilizopita ili kujua zaidi shughuli za msiba huu zinakwendaje na tunazidi kuwasihi tusaidiane na tujitolee katika kuhakikisha dola 4,000 zilizobakia zinapatikana. Mnaweza vile vile kufika nyumbani kwa familia ya Nestory Mwombeki Rweyemamu kutoa michango yenu, anwani ni: 40 East Sidney Avenue, Apt # 10C , Mount Vernon, NY 10550. Na namba ya simu ya nyumbani ni 914-667-6456.
 
Kwa kumalizia familia ya Nestory Mwombeki Rweyemamu inapenda kutoa shukrani za dhati kwenu nyote kwa kila msaada na ushirikiano mlioutoa na ule mtakaoutoa.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa. Amina.
 
Uongozi - Jumuiya ya Watanzania New York.
Next Post Previous Post
Bukobawadau