Bukobawadau

VIONGOZI MBALIMBALI WAUAGA MWILI WA MAREHEMU BALOZI FULGENCE KAZAURA KATIKA KANISA LA MT. PETER JIJINI DAR LEO

Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura likiwa ndani ya Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam tayari kwa Ibada maalum ya kumuombea Marehemu huyo iliyofanyika mchana wa leo kanisani hapo.Picha zote na Othman Michuzi.
Viongozi wa Kanisa hilo la Mt. Peter wakiwaongoza waomboleazaji kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa akiwaongoza waomboleazaji mbali mbali kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu. Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter, Osterbay jijini Dar es Salaam.

ENDELEA KUFUATILIA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Prof. Rwekaza Mkandala (mbele) Sir George Kahama,pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimfariji Mjane wa Marehemu pamoja na watoto wakati wa Ibada maalum ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura,iliyofanyika kwenye kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.
Familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura ikiwa kanisani hapo sambamba na waombelezaji wengine mbali mbali.
Watoto wa Marehemu Balozi Fulgence Kazaura wakizungumza jambo, pamoja na Mama yao (katikati).
Mtoto Mkubwa wa Marehemu Balozi Fulgence Kazaura, Kamugisha Kazaura akisoma risala fupi ya baba yake wakati wa Ibada Maalum ya kutoa heshima za mwisho,iliyofanyika mchana wa leo kwenye Kanisa la Mt. Peter, Osterbay jijini Dar es Salaam.
Mzee Samuel Tassa ambaye alikuwa ni mtu wa karibu la Marehemu Balozi Fulgence Kazaura, akimzungumzia namna walivyoweza kuishi pamoja katika kipindi chote cha Uhai wake.
Mwakilishi wa Mabalozi wastaafu nchini, Balozi Anthony Nyaki akitoa ujumbe wa Mabalozi wenzake namna walivyoguswa na msiba huo wa Mwenzao, Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.

Ibada ikiendelea kanisani hapo.
Mh. Mkapa akilishwa Mkate wa Bwana.
Prof. Mkandala akilishwa Mkate wa Bwana.
Sir George Kahama.

PICHA NA OTHMAN MICHUZI
Next Post Previous Post
Bukobawadau