Bukobawadau

CCM WAIBUKA KIDEDEA JIMBO LA KALENGA KWA ASILIMIA 79.4

ILIKUWA mwezi, wiki, siku, masaa na sasa limetimia ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa kumpata Mbunge wa jimbo la Kalenga, baada ya kuzoa kura kwa asilimia 79.4 dhidi ya wapinzani wao Chadema waliopata asilimia 20.1 na Chausta 0.51. Kwa nafasi hiyo, Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa amekuwa Mbunge mpya akichukua nafasi ya Mbunge aliyefariki jimboni humo, Dr William Mgimwa.
Matokeo ya uchaguzi huo, yanatoa nafasi nyingine kwa CCM kuweka rekodi ya kushinda chaguzi ndogo za ubunge katika majimbo mbalimbali yaliyokuwa nyameachwa wazi.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, CCM imeshinda kwa kura 22,943 dhidi ya kura 5,800 za Chadema huku chausta ikiambukia 143.
Ushindi wa jimbo la Kalenga, ni mwanzo wa kuanza mbio nyingine za uchaguzi katika jimbo la Chalinze.
Mwisho.(P.T)
Next Post Previous Post
Bukobawadau