MZEE JAMES RUGEMALILA ATOA MIL.200/- KATIKA MAHAFALI YA TATU YA SHULE YA SEKONDARI YA KAJUMULO GIRLS HIGH SCHOOL BUKOBA
Prof. Anna Tibaijuka kwa furaha akitoa neno.Kwa
niaba ya Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea na Mwana hisa wa “VIP
Engineering and Marketing Ltd” Mzee James Rugemalira aliyependa kuwa
nasi leo lakini akashindwa kutokana na majukumu mengine, tunayo furaha
kuwatangazia, kuwa VIP ataanzisha mfuko maalum wa kusaidia katika
kuboresha utoaji Elimu katika nchi yetu, utakaoitwa “Auleria Kobulungo
Muganda Memorial Education Foundation Trust”. Mfuko huu unaanzishwa kwa
heshima na kumbukumbu ya mzazi wetu mpendwa marehemu Ma Auleria
Kobulungo Muganda.
Mheshimiwa
mgeni rasmi, Tunayo furaha kutangaza kwamba shule yetu ya Kajumulo
Girls High school ndio itakuwa shule ya kwanza kufaidika na mfuko huu,
na leo, VIP kwa niaba ya “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education
Foundation Trust” imetoa jumla ya TZS 200 million (TZS 200,000,000) kwa
ajili ya kuwasadia baadhi ya watoto wasio na uwezo wa kujilipia lakini
wana sifa za kujiunga na kusoma katika shule hii.
Sehemu yaWanafunzi wa Kajumulo Girls High School wanaohitimu kidato cha 6 wakati wa kusherekea mahafali ya tatu katika shule yao.
Ni matarajio yetu kuwa mchango huu utawafikia walengwa, wale watoto wenye uwezo na nia ya kusoma, lakini wanatatizwa na karo pamoja na michango mingine ya shule.
Ni matarajio yetu kuwa mchango huu utawafikia walengwa, wale watoto wenye uwezo na nia ya kusoma, lakini wanatatizwa na karo pamoja na michango mingine ya shule.
Tutashirikiana
na Uongozi wa Shule na Wataalam wengine kuweka taratibu za uwazi
zitakazoongoza uteuzi wa watoto watakao faidika na msaada wetu.
Ninaisihi sana kamati itakayohusika na uchambuzi wa watoto wanaofaa kwa
msaada huu itende kazi yake kwa uadilifu ili wale watakaochaguliwa
kuhudumiwa wawe wale wanaostahili huduma hii.
Pia,
ni matarajio yetu kuwa mchango wetu utakuwa kichocheo kwa watu wengine
kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule yetu hii ili iweze kupiga hatua
zaidi katika jitihada za kutoa elimu bora kwa mtoto wa kike. Siku hizi
watu wengi wanaweka jitihada kubwa kuzungumzia matatizo, wakati wanaweka
jitihada kidogo katika juhudi za kuyatatua. Tukishirikiana kwa dhati
bila shaka tunaweza kupunguza matatizo ya watoto wetu.
Kwa
wale wanafunzi watakaohudumiwa na michango kama hii, ni mategemeo yetu
kuwa mchango huu utawaongezea bidii ya kusoma kwa kujiamini bila mashaka
kwamba watafukuzwa shule kwa kukosa karo au mahitaji mengine ya shule.
Tafadhali weka juhudi ili muweze kusoma vizuri, na mukimaliza shule
tuweze kuona matunda ya upendo wetu kwenu. Hakuna tunachodai kwenu, ila
mafanikio yenu katika maisha.
Baba Askofu Kilaini nae alitoa neno
Mkuu
wa Shule ya Kajumulo Girls High School Jospina Leonidace(kushoto) na
kulia ni Fr. Vitus Mrosso (Nyuma) katikati ni Mr. Adrew Kagya akiwa na
Balozi wa Climax Mjini Bukoba Mdau Rahym Kabyemela
Prof.
Anna Tibaijuka akiwa na Mgeni rasmi Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi. Edwina
Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank" kwa furaha
wakisikiliza Risala kutoka Wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita
Wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita(6) wakisoma Risala
Taswira,
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita wakisoma Risala mbele ya Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank, Mama Edwina Lupembe na
viongozi mbalimbali Meza kuu.
Risala ikikabidhiwa meza kuu
Sehemu ya Wazazi na walezi wa Wanafunzi
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha 6 wakitoa burudani yao
Raha ya kuhitimu Shule..
Wanafunzi wanaohitimu Shule hiyo ya Kajumulo Girls High School ya Wasichana wakicheza Ngoma yao
Ngoma ya kileo mchanganyiko wa Mtorona kaulule kwa ladha ya Skelewu
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank, Mama Edwina Lupembe akitoa neno.
Mr. Andrew Kagya akitoa neno.
Kwanza
kabisa ni kudhihirisha kwamba VIP inagawana ndoto (VIP shares the same
Vision) na mwanzilishi wa shule hii Prof. Anna Tibaijuka, ya kumkomboa
mtoto wa kike ili aweze kujitegemea yeye mwenyewe, wale anaowategemea na
hatimae kukomboa Taifa zima. Ni imani yetu (Conviction) kwamba njia
bora ya kumkomboa mtoto wa kike ni kumpa elimu bora.
Ni
njia ya kuwapa fursa watoto ambao hawana uwezo wa kifedha lakini wana
sifa zinazotakiwa kupata elimu bora. Ni wakati wa kuwaonesha watoto hawa
kwamba pamoja na ubinafsi unaongezeka katika jamii, bado kuna watu
wanaowajali na kuwathamini. Watu ambao wako tayari kuona hata wao
wanapata fursa ya kufanikiwa katika maisha. Watoto hawa wakitambua
vizuri thamani ya mchango huu, wakatambua thamani ya upendo wa Taifa
kwao, na hiyo itawajengea moyo wa kuwasaidia wale ambao hawana uwezo
wakiwa watu wazima.
Namna nzuri ya kufundisha upendo, ni kuonyesha upendo, na namna nzuri ya kuonyesha upendo ni kwa matendo
Ngoma kutoka Ngote Wilayani Muleba nayo ilianza kutumbuiza
Hakika Wanyayangilo wanatisha kwa kucheza ngoma.
Kwa hili linaloendelea kutoka Ngote hakika jirani zetu Wahamba mkajipange
Toka utawala wa Ntare, wahaya wametisha kwa kucheza ngoma.
Toka utawala wa Ntare, wahaya wametisha kwa kucheza ngoma.
Burudani ya Ngoma kutoka wanafunzi wa Kidato cha kwanza.
Uzinduzi wa Jarida la kila mwaka kwa Shule hiyo ulifuata.
Uzinduzi wa Jarida la kila mwaka kwa Shule hiyo ulifuata.
Kwa hisani ya Windhoek na Climax