Bukobawadau

SHUKRANI KUTOKA TANO LADIES!!

TANO Ladies wanatoa shukrani za dhati kwa watu mlioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhadhimisha sherehe  ya siku ya Wanawake Duniani 2014. Shukrani za pekee kwa Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula na wanawake Wajasiriamali walioshiriki kwenye maonyesho:Mitindo Nite, NASHONA,Taste of Tanzania,Farida Cartering,Little Ladies of Diaspora,SHINA INC ,IskaJoJo Studios,Computer Repair Services ,Nesi Wangu ,Bahari Deco.Crafts ,Marbella Events Inc ,Lucy Nombo,Erica Lulwakwa Glenn na Design by Salha Saleh. Mwisho ni akina baba na akina mama wote mliokuja kujumuhika nasi siku ya Jumamosi ,Machi 08. Hatuna cha kuwalipa,lakini wema wenu haujaenda bure! Ahsanteni sana kwa kuwa sisi pekee hatutaweza lakini kwa ushirikiano nanyi, tunaweza!Ahsanteni sana.
Kwa taswira zaidi ilivyokuwa mtembelee IskaJoJo Studios
http://www.iskajojostudios.com/Events/International-Womens-Day-March/
Next Post Previous Post
Bukobawadau