Bukobawadau

TASWIRA UZINDUZI RASMI WA KATIBA YA BUKOBA VETERANS NA KUPOKEA MSAADA WA JEZI KUTOKA NCHINI UJERUMANI CHINI YA UDHAMINI WA KINYWAJI BORA CLIMAX LEO MARCHI 30,2014

Naam! Kwa siku ya leo Jumapili Marchi 30,2014 ni hatua nyingine kwa  timu ya Bukoba Veterans ikiwa ni Uzinduzi  rasmi wa Katiba yake ,Sehemu kubwa ya Wanachama  wa Bukoba Veterans wamehudhulia Uzinduzi huu ulio ambatana na kupokea zawadi ya Jezi kutoka  nchini Ujerumani.
 Anaingia Ukumbini Mgeni Rasmi Bi Sakina Sinda ambaye ni Wakili wa Serikali mfawidhi Mkoa wa Kagera.
 Katibu wa Bukoba Veterans Ndg Rackson Kahabuka akitolea jambo ufafanuzi.
 Meza kuu wakimsikiliza Katibu Ndg Rackson Kahabuka,kutoka kushoto ni Fr Gerald Rugumila,Mgeni Rasmi Bi Sakina Sinda, Mwenyekiti Bukoba Veterans Ndg E. Nyambo mwisho ni Ndugu Chama Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA.
 Taswira kamili ya Meza Kuu ,pichani mmoja wa wahudumu akiendelea kutoa huduma ya Kinywaji cha Climax
Anaonekana Ndg Sued Juma Sued Kagasheki pichani kushoto
 Meza kuu yupo Bwana William Rutta wa Kiroyera Tours,katikati ni Fr.Mroso kama wanavyo onekana wakiteta na Afisa Utamaduni Manispaa ya Bukoba Ndg Rugeiyamu pichani kushoto.
 Mwenyekiti wa Bukoba Veteran's Sports Club Ndg E. Nyambo akiongea kuhusiana na mabadiliko kidogo ya ratiba ya siku ya leo kutokana na Mmoja wa wadau muhimu kupata dharula, hivyo anatoa fulsa kwa Ndg William Rutta kutoa Intro na kumkaribisha rafiki yake(Mgeni wetu wa leo)....Endelea kuwa nasi endelea kuipenda Bukobawadau Blog, Picha ndiyo kwanza inaanza!!
 Anaitwa Willy Rutta,kwa kutambua umuhimu wake katika Jamii tunapenda kumuita Mpambanaji Willy Kiroyera Rutta.
Mgeni wetu wa Leo ni Fr Gerald Rugumila rafiki mkubwa wa Ndg Willy Kiroyera Rutta.
 Ndugu Mwananchi pichani kushoto na Ndugu Yakubu kulia  Wanachama wa Bukoba Veterans wakimsikiliza Mgeni wetu wa Leo Fr Gerald Rugumila
 Sehemu ya Wanachama wa Bukoba Veterans.
 Fr Gerald Rugumila akikabidhi msaada wake wa Jezi kwa kapteni wa Bukoba Veteran's
Sports Club, Ndugu Mwinyi pichani katikati

Kapteni wa timu ya Bukoba Veteran's Sports Club akiendelea kupokea Msaada.
 Kwa umakini anaonekana akifuatilia kinacho endelea Mdau Mohamed Kassim.
 Mmanyema wa Uswahili Bilele,Ndugu Chama Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA, Akitoa shukrani kwa  msaada huo uliotolewa na kusema;ni kitendo cha kizalendo kilichofanywa na Fr Gerald Rugumila na anaamini kwamba wapo wadau wengi uko nje wenye kuweza kufanya kitu kama hiki.
Afisa Utamaduni Manispaa ya Bukoba Ndg Rugeiyamua akitoa neno na kuwapongeza Bukoba Veterans kwa wapo katika utaratibu mzuri na kitendo cha leo kinadhihirisha
 Lamgambo likilia ujue kuna jambo!!
 Ukisema burudani kwa bukoba veteran ndio umewagusa,hapo wakiongozwa na dancer matata wa Kakau Bend, Mbishi Moses Nyama akiwaongoza kufanya yake hakika ilikuwa raha isiyo kifani
 Kijana machachari Jerry ambaye pia ni mkurugenzi wa SHEMEJI INVESTMENT GROUP iliyopo mpakani Mtukula alifanya kazi nzuri katika kutoa maelezo yaliyokwenda shule,huyu ni mwanaveteran mahili kabisa,analipa michango yake akiwa wa kwanza kabisa na kazi ya U MC kwenye issue ya Veteran uwa anafanya bure,shida ni kuwa hatujui katika veteran uwa anacheza namba gani ?!!!
Bukoba Veteran's Wanatoa Sebene moja matata kwa ajili ya kumshukuru Mgeni wetu Leo.
 Mtata MC Jerry akiruka mangoma kwa staili za kule kwao upareni
Mpaka hapa kila kitu kinaenda sawa na hivi sasa kilichobaki ni uzinduzi wa Katiba.
Aliyesimama ni Mh.Matete mhusika mkuu katika Utaratibu wa kuandaa  Katiba ya Bukoba Veterans.
 Mdau Paulo Kadushi aka Paulo Mgalilaya na Mama Redempter Mwebesa maarufu kama Mama Maziku wao ni wajumbe wa Katiba ya Bukoba Veteran's Sports Club.
Katikati ni Katibu wa FC Balimi ndg Optaty Henry akiipitia Katiba ya Bukoba Veterans.
 Shughuli ya Uzinduzi huu umedhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd. Dar Es Salaam, kupitia kinywaji  maridadi  Climax(Non Alcoholic Energy Drink)
 Neno kutoka kwa Mgeni Rasmi Bi Sakina Sinda ambaye ni Wakili wa Serikali mfawidhi Mkoa wa Kagera.
 Kitendo kinacho endelea ni Uzinduzi Rasmi wa Katiba ya Bukoba Veteran's Sports Club.
 Mgeni rasmi Mama Sakina Sinda alitoa hotuba nzuri sana ila zaidi aliwahasa wanachama kuzingatia mazoezi maana ni mazuri kwa afya zao na pia ata ki uchumi inapunguza matumizi yasiyo ya lazima
 Mdau kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA akiwa makini kabisa na hotuba ya mgeni rasmi.
 Kijana Sugu wao kashai umuita Sugu lala,nae alikuwepo na Raster zake ili mradi tu kuweka mipango ya kaka zake wa veteran ikae kama ilivyopangwa chini ya Udhamini wa Climax.
 Ustaadh Moa na Bob Rama kwa mbele na kamanda Baragaza wa usalama barabarani wilaya ya Muleba ili mradi Veteran ipo kila Idara mpaka wakulima na wafugaji,ULINZI SHIRIKISHI POLISI JAMII
 Kutoka kushoni  ni Ndg Reuben Sunday, Mkurugenzi Mtensa na Bwana Sadi Idd wakiperuzi.
Pichani kulia ni Haji Sadick Galiatano, Mzee wa wagadi toka mwanzoni mwa 80 pia ni  Mwanachama wa Bukoba Veterans.
Wakiwa ndani ya Jezi Mpya.
 Ni fulsa sasa ya kupata Chakula kama anavyo onekana Mgeni Rasmi pichani.
Mwanamama Salome Chui na London jina London lilitokana  na mfumo wake wa maisha, maujanja yaka swaga na mtikiso wa maumbile plus Umjini kama wa mbele hivi.
 Bi Mainda Kassim mwanachama  Bukoba Veterans akipata huduma ya msosi.
 Ndugu Rajabu Paulini akifuatiwa na Ndugu Andrew Mutagobwa Kagya
 Huduma ya Chakula safi chini ya Udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd. Dar Es Salaam, kupitia kinywaji  maridadi  Climax(Non Alcoholic Energy Drink)
 Ndugu Sunday pichani akufuatiwa na Mdau Mugisha almaarufu Kingereza mzee wa mustachi bingwa wa drafti kata ya Bakoba
 Hakika vetetan imesheheni watu wa kila idara,nashawishika kumuulizia Dr.Mussa maana nasikia na yeye ni mwanachama hai kabisa
 Uzi wenyewe ndio huo umepigwa na Fr Mroso wa ntungamo seminari na Afisa utamaduni Manispaa Bukoba Mr..Rugeiyamu
Bukoba  Veteran wanasema hivi ukipewa na wewe jua kushukuru,hapo na wao wametoa zawadi ya Tshirt mpyaaa ili jina lao nalo lipeperuke mitaa ya Munich huko Germany
 Fr Gerald Rugumila amepokea kwa furaha zawadi hiyo
Katika picha ya  pamoja Mgeni Rasmi, mdhamini wetu wa Jezi na Wanachama.
MWISHO.


Next Post Previous Post
Bukobawadau