WANANCHI KIJIJI NYABIHOKWE -BWANJAI NI MFANO WA KUIGWA
"SISI WAWATA(Wanawake Wakatoliki Tanzania) huwa tunajitolea mara kwa mara kuwasaidia watu wasio na uwezo,ndio maana tuliona tumsaidie yule mzee na tunaendelea kusaidia hata kama tayari amefariki dunia),anasema Bi Aloysia Deogratias ambaye ni mwenyekiti wa WAWATA, kijiji cha
Nyabihokwe kata ya Bwanjai.
Leo hii wananchi zaidi ya 150 wa kijiji hicho wamejumuika kujitolea kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mzee Tryphone Juma(80)katika kitongoji cha Bukomola.ambaye sasa ni marehemu aliyefariki kwa ugonjwa 23.03.2014
"Mzee huyo alikuwa na kijana wake mmoja tu aliyejaliwa kumpata,aliondoka muda mrefu,na hivyo mzee huyo alihitaji msaada ambapo wanaukoo,WAWATA na sisi wananchi tulisaidia na sasa tunaikamilisha hii nyumba ili aishi kaka yake mkubwa (86)waliyekuwa wakiishi wote",amesema Jonathan Raphael ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji hicho cha Bukomola
Muonekano wa nyumba inayojengwa kwa nguvu za wananchi
Msemaji wa familia,Dauda Yusufu Katolelwa anasema hana cha kuwalipa wanakijiji hao bali kuwaomba waendelee na moyo wa upendo na umoja.
Pichani ni Ndugu na jamaa za marehemu Tryphone Juma.,mwenye kofia ni msemaji wa
familia Ndg Dauda Yusufu Katolelwa.
Sehemu ya viongozi wa WAWATA kijiji cha Nyabihokwe,wa kwanza kushoto ni mwenyekiti Bi Aloysia Deogratias.
Pichani ni mwenyekiti wa kitongoji cha Bukomola,Ndg Jonathan Raphael.

Ndugu wasomaji wa Bukobawadau BLOG, hii ni moja ya Changamoto kwetu sote tukiachilia mbali matatizo makubwa ya ukosefu wa huduma za afya
Hakika Maisha ya Kijijini ni Changamoto – Tuwakumbuke Wenzetu. Hii ndiyo nyumba waliojitolea wananchi katika kuisaidia familia ya Marehemu Tryphone Juma!!.
CREDID; MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi