Bukobawadau

MAN UNITED 1-1 BAYERN MUNICH 1 NI KAMA MANCHESTER UNITED YA ZAMANI

Bao la kuongoza la  Manchester United lililofungwa na Mchezaji Nemanja Vidic kwa kichwa Hakika usiku wa leo timu ya manchester united wanastahili pongezi,kwa kiasi kikubwa wameonyesha malengo,Mapema ya mchezo wamejaribu  kutengeneza nafasi kadhaa za goli,na wamepata goli la kuongoza kabla ya wapinzani wao.
Kipindi cha pili  United walianza kwa kufanya mabadiliko, ambapo alitoka Ryan Giggs ambaye akuonyesha msaada wowote kama kiungo na nafasi yake kuchukuliwa na Mchezaji Shinji Kagawa.
Ryan Giggs  hii  inaweza kuwa mechi yake ya mwisho katika Ligi ya Mabingwa ndani ya uwanja wa Old Trafford
Nafasi ya Waziya kujutia kwa Manchester United wakati Mchezaji Danny Welbeck (katikati) anashindwa kujua anacho kifanya pale shuti lake linapo okolewa na mlinda mlango wa Bayern Munich,Manuel Neuer
 Mashabiki Bayern Munich wakionyeshavitambaa vya rangi yao ndani ya Uwanja wa Old Trafford.
 Mbinu za kimchezo ni siri,Pichani anaonekana meneja wa Manchester United David Moyes akitoa ishara kwa wachezaji wake uwanjani 
 Kipa wa Manchester United David de Gea katika majukumu yake ya kuokoa mpira.
 Hekaheka langoni mwa Manchester United kama anavyo onekana Mchezaji Rio Ferdinand akiokoa.
Mchezaji waManchester United Antonio Valencia akimfanyia undava mchezaji wa  Bayern, Philipp Lahm.
 Mwamuzi Carlos Velasco Carballo anatoa kadi ya njano kwa mchezaji Antonio Valencia wa Manchester United kwa mchezo mbaya ,pichani wachezaji wachezaji wa Bayern wakionyesha kuchukizwa na kitendo hicho
Meneja wa Zamani wa Manchester United  Sir Alex Ferguson anaonekana akiangalia saa yake ikiwa ni kipindi cha kwanza cha mchezo.
 Hekaheka za uwanjani,Danny Welbeck akimchezea vibaya Mchezaji  wa Munich Javi Martinez
 Mchezaji wa Bayern Munich,Bastian Schweinsteiger akishangilia  baada ya kufunga baola kusawazisha 1-1 katika uwanja wa Old Trafford
 Mchezo wa leo tumeshuhudia Mchezaji Bastian Schweinsteiger wa Bayern Munich akipata kadi nyekundukatika dakika ya mwisho
 Mchezaji Toni Kroos (kulia) akiteta jambo na Kocha  Pep Guardiolawakati anafaniwa mabadiriko
 Meneja wa Manchester United ,David Moyes akitafakali hatima yake kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya makubwawa Ujerumani Bayern Munich
 Kocha Mkuu wa Bayern  Guardiola  anaona sare ya Ugenini ya bao 1-1 inamanufaa kwake 

 Ni shidaaa, Mchezaji Arjen Robben akifanya yake katika harakati mbele ya Shinji Kagawa (kushoto) na Phil Jones 
 Kocha wa Bayern Munich  Pep Guardiola (kushoto)akitikisa kichwa juu chini wakati anapeana  mikono na David Moyes meneja wa Manchester United.
Next Post Previous Post
Bukobawadau