Bukobawadau

WANAHABARI WA MWANACHI COMMUNICATION KANDA YA ZIWA WAPIGWA MSASA

Aika Massawe.MWANZA MARCH,16,2014

Kampuni ya gazeti la Mwananchi imejipanga kupanua wigo wa kuandika habari kutoka kanda ya ziwa kwa kutoa vipaumbele sita ili wananchi wapate habari zinazoelezea changamoto na fursa katika sekta zinazoweza kukuza uchumi

Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi  Bakari Machumu amesema hayo leo kwa wanahabari  wanaoandikia gazeti hilo kutoka mikoa ya  kanda ya ziwa wakati wa semina elekezi juu ya mipango ya upanuzi na  utoaji huduma kwa wananchi

Machumu amesema kuwa katika habari za kanda ya ziwa kipaumbele ni  katika sekta ya  uchimbaji madini ,kilimo , uvuvi,siasa ,biashara na utalii pamoja na manufaa yake kupitia njia za  ujasiliamali ndani ya jumuia ya afrika Mashariki.

Alisema Wanahabari watumie uzalendo wa uhuru wa habari kwa kuepuka kuandika habari za kushusha hadhi za watu pamoja a uchohezi na kusababisha uvunifu wa sheria endapo hakutakuwa na ushahidi wa kutosha  kuhusu taarifa zao 
“Lengo la upanuzi wa habari mikoa ya kanda ya ziwa ni kueleza hali ya uwajibikaji katika  kuleta maendeleo changamoto za kiutendaji katika serikali, vyama vya siasa na utawala bora  kisha upatikanaji wa huduma za jamii”.alisema Machumu

Awali  Meneja Utawala na sheria wa Mwananchi Communication Ltd Doris Maliale jana  alisema habari zenye migogoro huleta hasara kwa Taasisi ama  kampuni kwa kuwepo mashataka ya kesi ama malalamiko mahakamani.

Alisema madhara makubwa yanapotokea hukumba watumishi mbalimbali wa  taasisi kuanzia mwandishi hadi mchapishaji habari ambapo rasimali fedha hutumika na kuharibu mipango ya uzalishaji na kuibua migogoro ndani ya jamii

 “Uandishi unaweza kumpandisha mtu hadhi  yake ama kuishusha hivyo kunahitaji uangalifu katika kufanya kazi kwenye mazingira ya habari ikiwa ni pamoja na kubainisha source husika kuliko kutaja kundi la watu ama kampuni”.Alisema

Alisema katika kutumia maadili ya uandishi wajihadhari na kuwatishia watuhumiwa wa mambo mbalimbali kwenye taasisi na lazima kukusanywe ushahidi wa pande mbili na kujiridhisha na ukweli utakaokuwa umetolewa

Kwa upande wake mhariri mkuu wa MCL Theophil Makunga alisema kampuni ya MCL imejipanua kwa kuingia ubia na kampuni ya  Jamana  kuchapa gazeti hilo na kusambaza nakala kwa wasomaji wengi kanda ya ziwa ifikapo Aprili mwaka huu.

Alisema mpango wa kuanza kuchapicha nakala hizo tayari umekamilika kinachosubiliwa ni Tanesco kusambaza umeme kwenye kiwanda cha uchapaji na magazeti yatakayochapishwa ni mwananchi mwanaspoti na the Citzen

“Tumejipanga kuhudumia wananchi wetu kupata habari kwa wakati na mipango inapanuka mwaka jana tulianzisha breacking news na tunatarajia hata kuwa na Tv na radio pia  kuingia zaidi katika website kufikia mwakani”.  Alisema Makunga

Naye  mhariri  wa habari za kanda ya ziwa Midraji Ibrahimu alisisitiza wanahabari kuhakikisha wanafika kwenye eneo la tukio na kutuma habari zenye uhakika ili  jamii iendelee kuwaamini na wao kufanya kazi katika mazingira ya usalama.

Alisema miongoni mwa habari zenye manufaa kwenye jamii ni zile ambazo hazitaleta hisia za ubaguzi ama uchochezi wa kidini kikabila jinsia na unyanyapaa na kuvunja mahusiano kati ya jamii na vyombo vya dola katika utawala bora.
 Maneja utawala na sheria Doris Malealle
 Baadhi ya wanahabari wa kanda ya ziwa –Mwananchi
 Kushoto ni Thophil Makunga na kulia ni Midraji Ibrahimu Mhariri habari kanda ya ziwa- Mwananchi
 Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Human Resource wa mwananchi Aika Massawe wa Mwananchi akitoa mada ya uadilifu kiutendaji
 Na Shaaban Ndyamukama
Next Post Previous Post
Bukobawadau