BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AHAIDI UWEKEZAJI MKUBWA TOKA CHINA KATIKA MKOANI KAGERA
Balozi Lu Youqing wa Kwanza Kushoto Akiwa na Mkuu wa Mkoa Mhe.
Massawe Katikati na KatibuTawala wa Mkoa wa kagera Bw. Nassor mnambila.
Balozi Lu Akiwa na mkarimani Wake Bw.Ren
Mkuu wa Mkoa wa kagera Mhe Massawe Akimkaribisha Balozi wa China Nchini Tanzania Dk. Lu Youqing Mkoani Kagera.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila Akiwasilisha Mada kuhusu Fursa za Uwekezaji Mkoani Kagera
Balozi Lu Youqing Akifurahia Jambo
Mkoa wa wa Kagera ukiongozwa na Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe umefanya mkutano wa uwekezaji na nchi ya China iliyowakilishwa na ujumbe ulioongozwa na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Younqing.
Balozi Lu Akiwa na mkarimani Wake Bw.Ren
Mkuu wa Mkoa wa kagera Mhe Massawe Akimkaribisha Balozi wa China Nchini Tanzania Dk. Lu Youqing Mkoani Kagera.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila Akiwasilisha Mada kuhusu Fursa za Uwekezaji Mkoani Kagera
Balozi Lu Youqing Akifurahia Jambo
Mkoa wa wa Kagera ukiongozwa na Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe umefanya mkutano wa uwekezaji na nchi ya China iliyowakilishwa na ujumbe ulioongozwa na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Younqing.
Balozi Lu Younqing na ujumbe wake walifika mkoani Kagera
tarehe 16/04/2014 kwa lengo la kuhudhuria mkutano wa pamoja na mkoa wa
kuhusu uwekezaji katika sekta mbalimbali na kujionea fursa zilizopo mkoani hapa
kwa ajili ya uwekezaji.
Akimkaribisha Balozi Lu Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Mhe. Massawe alimshukuru kwa kufikiria kuja mkoani hapa kujionea
mwenyewe fursa zilizopo na kumhakikishia ushirikiano mzuri kwa wawekezaji toka
nchini China kuja kuwekeza na kuinua uchumi wawananchi wa mkoa wa Kagera .
Katika mkutano huo wa pamoja wa
uwekezaji mkoa wa Kagera uliwasilisha mbele ya Balozi Lu na ujumbe wake fursa
muhimu na Sekta mbalimbali za kuwekeza ili kuinua uchumi wa mkoa na taifa kwa
ujumla kama ifuatavyo:
Sekta na fursa hizo ni pamoja na Viwanda, Kilimo cha umwagiliaji,
Uzalishaji na usafirishaji wa ndizi, Ufugaji wa kisasa, Usindikaji wa nyama na
maziwa, Uvuvi na ufugaji wa samaki wa kisasa, Sekta ya uchimbaji madini, Sekta
ya utalii na ukarimu, Usafirishaji, ufugaji wa nyuki na usindikaji wa asali.
Fursa nyingine ni pamoja na Michezo
na burudani, pia kuwekeza katika huduma za jamii kama Haspitali, Shule, Vyuo
vya elimu ya Juu na Ufundi. Hizo ni Baadhi ya fursa na sekta ambazo
zinapatikana mkoani Kagera katika sekta ya uwekezaji.
Aidha fursa za kuwekeza haraka
ambazo zipo tayari kwa sasa ni Kilimo cha mahindi na mpunga katika Bonde la mto Ngono Wilayani
missenyi, Ujenzi wa nyumba za kisasa katika manispaa ya Bukoba, Ujenzi wa
Bandari ya kisasa Rwagati Kemondo Wilaya ya Bukoba, na Ufugaji wa kisasa
wa Samaki Ruhanga Wilayani Muleba.
Balozi Lu baada ya kusikiliza
maeneo ya uwekezaji alisema kuwa mkoa wa
Kagera ni sehemu nzuri sana ya kuwekeza na kuinua uchumi wa wananchi na taifa
kwa ujumla pia alisema Tanzania kwa inahitaji soko la bidhaa zake ili iweze
kupiga hatua katika uchumi.
Balozi Lu alisema atahakikisha
kuwa anawashawishi wawekezaji toka nchini China wanakuja kuwekeza katika sekta
mbalimbali hasa kwenye mkoa wa Kagera. Pia alisema kuwa mkoa wa Kagera
umebarikiwa fursa nyingi za uwekezaji kuliko mikoa mingi ya Tanzania
“Mwezi Juni 2014 Nchi ya China itafanya mkutano
mkubwa wa uwekezaji nchini Tanzania na Mkutano huo unatarajiwa kuwa na
wafanyabiashara wapatao 100 kutoka China kwa hiyo nitahakikisha mkoa wa Kagera
unashiriki na nitawashawishi wawekezaji
hao kukubali kuwekeza mkoni Kagera.”
Alisema Balozi Lu.
Katika hatua nyingine Balozi Lu
alihaidi kuwashawishi na kuwaalika wafanyabiashara wa Kichina Kuja kushiriki
katika maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane mwaka huu 2014 Mkoani Kagera ili kuweka ushindani na
kubadilishana ujuzi wa biashara kati ya China na Mkoa wa Kagera.
“Tutayafanya yote hayo ili kuinua
uchumi wa wananchi wa mkoa wa Kagera kwasababu Tanzania ina urafiki mkubwa na
Nchi ya China zaidi ya Miaka 50 iliyopita na rafiki wa kweli ni Yule
akusaidiaye kwenye shida, tutashirikiana kuwekeza na kutafuta masoko ya bidhaa
za mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla .” Alimalizia Balozi Lu.
Waandishi wa habari Wakiwajibika Kupata Habari kwa Balozi Lu Youqing.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014