Bukobawadau

HII NDIYO NYUMBA YA KISASA ILIYOPO KIJIJINI BUGANGUZI YENYE SIFA NA VIGEZO STAHILI

Naam!Kwa mara nyingine libeneke la Bukobawadau linakuletea taswira kamili  ya moja kati ya nyumba iliyopo kijijini Buganguzi Wilayani Muleba.Hii ni nyumba kali iliyopo shambani kabisa, iliyojengwa kisasa kwa  kuzingatia ramani, mazingira na ubora unaotakiwa kwa kila sehemu ndani ya nyumba hiyo..
Utapata kuona sehemu ya nje na ndani ikiwai nyingine kukuonyesha taswira ya nyumba hii ya Mdau Alex Mutiganzi iliyopo Kijijini  Kabulala-Buhanga  ndani ya Kata yaBuganguzi umbali wa km 2 kutoka Buganguzi  Center.
Swala la huduma ya maji hakika limezingatiwa
Sehemu ya nyuma ya Nyumba hii ina Garage 1 ya magari, vyumba viwili vya kulala vya kulala, Chumba cha GYM  kwa ajili ya mazoezi.
Usawa wa ukuta wa nyumba ya mbele, kwa kutokea
Nyumba hii inauwanja wa Basket Ball, na eneo kubwa la maegesho ya magari zaidi ya kumi.
 Upande wa kulia wa nyumba hii,kuna vyumba viwili na kila chumba ni self contain,pia kuna sebule iliyokamilika kwa ajili  ya mgeni husika,pichani unaonekana mlango kwa ajili ya kuingia au kutoka.
 Muonekano wa mbele wa nyumba hii ,hapa ndio tunaanza kupata kitu kwa ajili yetu na kwa kizazi kijacho,libeneke la Bukobawadau Blog linaguswa na rangi husika ya nyumba hii.
 Sehemu hii ni nusu ya uwanja wa mbele wa Nyumba hii.
 Nyumba hii ina sebule/Sitting room tatu kwa matumizi tofauti,na dinning room moja
Sitting room ya pili hiyo ni general kwa mambo ya ndani .design na mapambo,mitindo mapambo
 Sitting room ya pili hii nikama Ukumbi wa Video,kwa ajili ya kutazama mpira na ni
maalum wa kutazama filamu

 Hapa ni Sitting Room

Muonekano wa Sebule kubwa /general
Hakika nyumba hii ndani kuna fully equiped yani kila kitu na full a/c, maji moto na baridi
 Huu ndio mlango wa kuingia katita vyumba viwili vya wageni ,kutokea ndani,maelezo ya vyumba hivi yametolewa katika picha za mwanzoni ikiwa kila chumba ni self contain,pia kuna sebule iliyokamilika kwa ajili  ya mgeni husika.
 Sitting room ya mwisho ambayo ni maalum kwa ajili ya Mwenye nyumba anapokuwa na maongezi ya falagha.
Ndani ya Nyumba  hii kuna chumba cha maktaba na sehemu ndogo ya vinywaji/kaunta ya ndani
 Vifaa mbalimbali vya mazoezi.
 Muonekano wa Gym kwa ajili ya Mazoezi.
  Yote juu ya yote ni simulizi lililopo Master Bed room, ambapo  mwanalibeneka wenu sikubahatika kuingia baada ya Camera yetu yenye uwezo wa kawaida kuishiwa Charge.
  Mabanda ya mifugo mbalimbali
Eneo kubwa nyuma la myuma Mdau Alex Mtiganzi anajishughulisha nalo kwa  ufungaji mbalimbali ikiwemo mifugo mbuzi, bata, kuu, sungura eneo kubwa ni kwa ufugaji wa Nguruwe.
 Mdau Alex Mutiganzi pichani(kulia)akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Massawe mara alipofika nyumbani kwake kukagua mradi wa ufugaji
Vyakula vya mifugo.
 Aina ya taa zikiangaza migombani, pembezoni mwa uzio wa nyumba hii
 Huko jikoni mambo yako hivi kuna sinki na kichujio chake cha kati pako kamili .maswala kama mabomba ya maji moto na baridi
Nyumba ina jiko la kisasa lenye mpangilio unaotakiwa ikiwemo friji la kisasa kabisa na
deep freezer "jokofu"

 Kwa mbali kushoto tofauti na nachini ya kabati zilizobeba sinki kuna vifaa vya usafi kama sabuni na sponji , katikati inaonekana meza ya chakula,pembezoni kulia ni  shelfu za vyombo za wazi zilizo kwa juu kidogo na kwenye hizi kabati za chini yake hifadhi masufuria na vikaangio
Taswira muonekano kati ya nyumba  hii na eneo lake la nyuma
Shamba lililopo katikati ya eneo maalum kwa ajili ya ufugaji, pichani kulia ni mabanda ya kuandalia chakula cha mifugo
 Bustani safi yenye kupendeza
Kutoka ndani ya Nyumba Nyumba hii yenye vyumba kama 5, mabafu 4, Ukumbi wa Video, Uwanja wa basketballs, Gym kwa ajili ya mazoezi na eneo kubwa la maegesho
Sehemu ya wadau kijijini Buganguzi wakicheck na Camera yetu.
 Pichani kushoto ni Mdau Mc Baraka akiteta jambo na Mkuu wa mkoa Kagera(katikati) Mhe.Kanali mstaafu Fabian I. Massawe,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba,Mh.Lembris Kipuyo .
 Moja kwa moja kutoka Kijijini Buganguzi
Tunatoa shukrani kwako mdau msomaji kwa kuendelea kutembelea mtandao wetu!!Next Post Previous Post
Bukobawadau