Bukobawadau

FULL TIME:REAL MADRID 1-0 BAYERN MUNICH Goal: Benzema 19.

 Mchezo nusu fainali ligi ya mabingwa Ulaya usiku wa leo,unamalizika kwa kioja cha aina yake mnamo muda ya nyongeza dakika 90+2, Ni pale mchezaji wa Buyern Mario Mandzukic alipo pata nafasi ya wazi na kumsogezea pande Philipp Lahm naye akaminya kwa mwenzake Thomas Muller, Muller akiwa katika malengo ya kupiga mpira ,anafanya kujikwatua kwa kisingizi kwamba Xabi Alonso kamchezea vibaya katika eneo la hatari,lengo lake ikiwa ni kupata penati 
Goaaaall;Karim Benzema anaipatia Madrid bao la kwanza ikiwa ni dakika ya 19.  
 Benzema akishangilia bao la kuongoza mbele ya mashabiki Real Madrid,Madrid 1-0 Buyern
 Pichani anaonekana Kuchanganyikiwa mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, baada ya kukosa bao la wazi ikiwa ni nafasi ya pili kwake
Hekaheka  mbalimbali, anaonekana mchezaji waBayern Munich Philipp Lahm akijaribu kumtoka mlinda mlango wa Real Madrid  Iker Casillas akiwa chini.
 Mwamuzi Howard Webb katika  majadiliano Mchezaji wa  Bayern Munich  Arjen Robben
Mchezaji wa  Bayern  Philipp Lahm (kushoto) akijaribu kuruka viunzi dhidi yaIsco wa Madrid
Anaonekana kocha wa Bayern Munich , Pep Guardiola  akitoa ishara ya malalamiko  kwa mwamuzi baada ya mchezaji wake  Philipp Lahm (aliyechini ) kukwatuliwa na Isco wa Real Madrid
Akiwa katika maumimu!! anaonekana Mwamuzi Howard Webb akidhibitisha kama kweli kaumia dhahiri mchezaji Pepe wa Real Madrid 
 Mchezaji Pepe wa Real Madrid akitoa ishara ya kuhitaji  matibabu
 Cristiano Ronaldo (kulia) akifuatilia namna  shuti lake linavyo okolewa na kipa Manuel wa Bayern 
 Mshike mshike kati ya mchezaji Gareth Bale (kulia) na Mchezaji wa  Bayern, Lahm
 Kinachotakiwa ni mwelekeo sahihi: ndivyo anavyo onekana Kocha wa Bayern Munich  Pep Guardiola akitoa  maelekezo kwa Arjen Robben.
Ni kizuri kama dhahabu: huu ndio muonekano wa kiatu kipya alichokitumia  Cristiano Ronaldo uwanjani usiku wa leo  muda huu anaingia Gareth Bale kuchukua nafasi ya Ronaldo hii ni baada ya Pepe kuumia.
Pichani mmoja wa madoo,shabiki wa Real Madrid anaangaika kuzoom camera yake kupata picha.
 Hivi ndivyo alivyo pendeza mwanadada msaidizi wa timu ya Bayern Munich .
Next Post Previous Post
Bukobawadau