Bukobawadau

KAGERA SUGAR NGUVU SAWA NA SIMBA 1-1 UWANJA WA KAITABA LEO APRILI 5,2014

Ligi kuu soka Tanzania Bara leo imetimua vumbi katika Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba,mechi ya leo kati ya Kagera Sugar na Simba ambapo Simba imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Kagera Sugar.
 Kwa matokeo ya leo,kupata Sare kunazidi  kuididimiza timu ya Simba na inawezekana kabisa Simba ikaingia katika wakati mgumu hata kupata nafasi ya nne mwishoni mwa ligi hii.
 Mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa Kanali Mstaafu F. Massawe ni pichani katikati, kushoto kwake ni Kanali Mstaafu Issa Njiku ambaye ni Mkuu wa Wilaya Mishenyi na kulia ni Ndugu Chama Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA
 Waitu tulio, karibu sana Bukoba.
Wachezaji wakiendelea kusalimiana
 Benchi la Kagera Sugar.
 IT manager Simba Sports Club Mdau Edbertious Mtawala maarufu kama(African Hank Mood)akiteta jambo na Katibu Mzee Issa Masharubu
 Katikati ni  Abdulrazak Majid mtangazi 88.5 Kasibante Fm Radio Bukoba akirusha matangazo moja kwa moja kutoka Uwanjani Kaitaba,Abdulrazak Majid ni mtangazi ni moja ya watangazi wakali nchini mwenye  uwezo,bidii na juhudi binafsi kazini.


  Kikosi kamili cha wachezaji wa Simba,Ivo Mapunda 22 Nassor Masoud 2 Omary Salum 4 Henry Joseph 14 Donald Mosoti 5 William Lucian 3 Twaha Ibrahim 27 Said Hamis 13 Zahoro Pazi 7 Uhuru Selemani 10 Edward Christopher 19
 Kikosi cha Wachezaji wa Kagera Sugar.
Waamuzi wa mchezo huu


Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini hapa, Simba ilianza kupata bao lake katika dakika ya 35 kupitia kwa mchezaji wake Zahoro Pazi lakini wenyeji Kagera wakasawazisha katika dakika ya 61.
 Wachezaji wa Kagera Sugar wakiingia uwanjani kukamilisha ngwe ya kipindi cha pili
 Mlinda Mlango wa Simba Ivo Mapunda akiangaika langoni
 Ivo mapunda akipata matibabu
 Kikosi Kazi cha Kagera Sugar Baada ya kupata bao la kusawazisha.
 Wazalendo wa Kagera Sugar katika hali ya furaha.
 Kaka Mkuu E. Nyambo na Ndg Richard wakifuatilia Soka.
 Simba imecheza mechi hiyo bila ya mshambuliaji wake Amissi Tambwe raia wa Burundi na beki Mganda Joseph Owino ambao ni wagonjwa.
Harakati za wachezaji wa Simba.
Kona kuelekea langoni mwa Simba.
 Vumbi likiendelea kutimuka uwanjani Kaitaba.


Soka safi kutaka kwa Vijana wa Kagera Sugar, wenye Jezi Nyekundi.
 Kikosi kazi cha Kagera Sugar  ambacho kimecheza soka la kisasa na kuwachanga Wachezaji wa Simba.


Mchezaji wa Kagera Sugar akimlalamikia muamuzi wa pembeni.
 Ivo Mapunda 
Nje ya Uwanja wa Kaitaba, Mtaa wa majumba 9,mashabiki wakijing'amuzi.
Mr Byamungu shabiki wa Soka, na kiroba mkononi.
Katika kushow love mbele ya Camera yetu wanaonekana Wanazi wa Kagera Sugar, wakimpeti Mwanamama mnazi wa Simba.
 Waleee Juu ya Miti, wakiendelea kufuatilia kilichokuwa kinajiri katika uwanja wa Kaitaba
Azam Media wakiendelea na kazi
Jukwaani wadau wakiendelea kufuatilia Soka.
 Kamanda Balagaza wa Usalama barabarani na Ndugu Gwaru kamati wa kikosi cha Mizinga wakifuatilia soka.
Sehemu ya mashabiki Jukwaa la Kagera Sugar.
Super Self Mkude akifuatilia Soka
 Katikati ni Rais wa Kombora Fc  ya Mjini hapa, kulia ni Ndg Dati Kasabila.
Jukwaa la Balimi
Mwanalibeneke Jamal Jamco Kalumuna.
 Sehemu ya wadau wa Soka Mjini hapa.
Mwanadada akifuatilia kile kinacho endelea ndani ya Uwanja wa Kaitaba.
 Anaonekana Ndugu Majid wa Mutukula
 Kijana Edbertious Mtawala Mtaalamu wa maswala ya IT wa timu ya Simba akibadirishana mawazo na Ndugu Hanas(kulia)
Anaitwa Mdau Dume pichani
 Taswira kamili yaliyojiri Uwanjani Kaitaba kwa jioni ya leo, Kagera 1-1 Simba.
 Mchezaji wa Simba akiwa amepata 
 Simba imecheza mechi ya leo bila ya mshambuliaji wake Amissi Tambwe Raia wa Burundi na beki kutoka Nchi Jirani ya Uganda maeneo ya Kalisizo Joseph Owino wanaosumbuliwa na Maladhi.
Bukobawadau Blog ikiendelea kukuangazia moja kwa moja kutoka  ndani ya Uwanja wa Kaitaba


Kanjanja pichani ni Ndugu Rama Home Boy Kashai.
Majumba 9,jirani kabisa na Uwanja wa Kaitaba.
Ndani ya Kaitaba jioni ya leo weengine walionekana wakiwa wamekwea juu ya miti ,wengine kupalamia kuta za Uwanja hii yote ni katika mchakato wa  kuweza kuuona mechi hii
Jukwaa maaarufu kwa Jina la Golani/ Balimi
Uncle Thomas Kashai.
 Kagera Sugar vs Simba SC Starting: Ivo Mapunda 22 Nassor Masoud 2 Omary Salum 4 Henry Joseph 14 Donald Mosoti 5 William Lucian 3 Twaha Ibrahim 27 Said Hamis 13 Zahoro Pazi 7 Uhuru Selemani 10 Edward Christopher 19 Substitutes: Yaw Berko 18 Hassan Hatibu 29 Awadh Juma 16 Ally Badru 21 Ramadhani Singano 11 Ramadhani Chombo 8 Haruna Chanongo 6


Next Post Previous Post
Bukobawadau