RULENGE KANAZI NA NYAMIANGA WILAYANI NGARA KUPATA HUDUMA YA UMEME
Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu
WANANCHI wa Tarafa za Rulenge Kanazi
na Nyamiaga wilayani Ngara Mkoani Kagera wanatarajia kusambaziwa huduma ya
nishati ya umeme baada ya Rais Kikwete
kutoa ahadi kwa wananchi wa tarafa hizo
katika ziara yake mwaka jana.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu
amesema mpango wa kusambaza umeme huo
utaanzia kijiji cha Djululigwa hadi Rulenge kupitia wakala wa umeme vijijini
REA ambapo mkandarasi kutoka D’Salaam kaishawasili wilayani humo
Kanyasu amesema kuwa mara baada ya
usambazaji umeme katika mji wa Rulenge na maeneo jirani atasambaza umeme huo
kutoka mjini Ngara hadi Rusumo na kutoka Rusumo hadi K9 kuelekea mji wa Benaco
na baadaye kata ya Mugoma.
“Rai yangu ni kwamba usambazaji
wa umeme wananchi wasikwamishe juhudi za
serikali kwa kudai fidia kwenye maeneo zitakaposimikwa nguzo na kupitisha
nyaya badala yake watoe ushirikiano kwa
wakandarasi”.Alisema Kanyasu
Aidha amewataka wananchi kuhakikisha
hawajengi kwenye hifadhi za barabara kuu zitakapopita nguzo na nyaya hizo na
watumie nishati ya umeme kwa manufaa ya kukuza maendeleo na kuanzisha miradi ya
ujasiliamali kujiongezea kipato
Aidha alisema Rais Kikwete alitoa
ahadi ya kuondoa kero ya maji katika mji wa Ngara na vitongoji vyake na tayari
Tsh.150 mil zimefikishwa katika idara ya mamlaka ya maji ili kununua mashine
mbili na kufungwa kwenye chanzo cha maji
Alisema taasisi za serikali katika
mji huo hasa polisi na magereza zinadaiwa ankra za maji zaidi ya Tsh.20mil
hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha fedha hizo zinalipwa ili kuepuka
kukwamisha uendeshaji na utoaji huduma kwa wateja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM
wilayani humo Hadson Bagege amesema miradi hiyo ya umeme na maji haina budi
kusimamiwa kwa ukaribu kuepuka ubadhilifu wa fedha za serikali na kutoa huduma
itakayoleta maslahi kwa jamii
Wilaya ya Ngara ina jumla ya vijiji
72 na wananchi wanaopata nishati ya umeme wa mafuta ni walio katika mji wa
Ngara kuelekea barabara kuu iendayo mji wa Kabanga kuelekea nchini Burundi
Ilielezwa kuwa 67 % ya wananchi wilayani humo wanapata
huduma ya maji safi na salama hasa vijiji vilivyofanikiwa kupata miradi ya maji
kupitia ufadhili wa benki ya dunia na 33% wanachota maji kwenye mito na visima
NGARA: Na Shaaban Ndyamukama