KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akikagua Gwaride Maalum mara baada yakuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigali nchini Rwanda
Rais Museveni amewasili Mjini Kigali kwa ajili ya kushiriki shughuli ya maadhimisho ya Miaka 20 ya Mauaji ya kimbari Rwanda ya mwaka 1994 yaliyofanyika leo Aprili 7,2014.
Rais Kagame katika picha na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta,mapema mjini Kigali.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon akiongea na Rais Kagame amesema;"Nimefika hapa kuupongeza Uongozi wa Rais Paul Kagame ambaye ameiongoza nchi hii kwa kipindi cha miaka 20 , Ameweza kufanya mambo mengi ya kuigwa, Kijamii,kiuchumi, Demokrasia na kulinda na kuheshimu haki za binadamu , natumaini huu ni mfano wa kuingwa kwa nchi nyingine,Dhamira yangu kama Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ni kuwashukuru wananchi wa Rwanda na kuupongeza Uongozi wa Rais Kagame "
MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA
Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yalikuwa mauaji ya kihalaiki mnamo mwaka wa 1994 ambapo Watutsi na Baadhi ya watu wa kabila la Kihutu waliuliwa na serikali iliyosimamiwa na viongozi wa Kihutu.Katika kipindi cha takriban siku 100, kuanzia kuuliwa kwa Habyarimana na Ntaryamira mnamo tarehe 6 Aprili hadi katikati mwa mwezi Julai, angalau watu 500,000 waliwawa, au karibu asilimia 20% ya idadi ya watu nchini Rwanda wakati huo.
Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yalikuwa mauaji ya kihalaiki mnamo mwaka wa 1994 ambapo Watutsi na Baadhi ya watu wa kabila la Kihutu waliuliwa na serikali iliyosimamiwa na viongozi wa Kihutu.Katika kipindi cha takriban siku 100, kuanzia kuuliwa kwa Habyarimana na Ntaryamira mnamo tarehe 6 Aprili hadi katikati mwa mwezi Julai, angalau watu 500,000 waliwawa, au karibu asilimia 20% ya idadi ya watu nchini Rwanda wakati huo.
Ujumbe wa majaji wa Ufaransa Jumamosi waliwasili mjini Kigali kwa lengo la kuchunguza chanzo cha mauaji ya kimbari ya Rwanda na kuanguka kwa ndege iliyokuwa imembeba Juvenail Habyarimana rais wa wakati huo wa Rwanda. Kuuawa Habyarimana April 6 mwaka 1994 kulikuwa chanzo muhimu cha mauaji ya kimbari nchini humo. Kuhusiana na kuuawa Habyarimana, Wahutu wenye misimamo ya kufurutu mpaka walihusisha tukio la kutunguliwa ndege yake na wapinzani wa Kitutsi na kulitumia kama kisingizio cha kuanzishia mashambulio na mauaji makubwa na ya kutisha dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye misimamo ya wastani. Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yaliendelea kwa muda wa siku 100 hadi hali ya mambo ilipodhibitiwa na vikosi vya waasi wa wakati huo wa RPF, wapiganaji wake wengi wakiwa ni Watutsi.


Kwa utaratibu huo Kamisheni Huru ya Kitaifa ambayo iliamuriwa na serikali ya Kigali ikusanye nyaraka na ushahidi unaothibitisha nafasi ya Paris katika mauaji ya Rwanda, ilitayarisha nyaraka zilizofichua jinsi Ufaransa ilivyoshiriki katika mauaji hayo, ambayo yalipewa jina la "Jinai za Watenda Jinai". Kwa mujibu wa ripoti ya kamisheni hiyo, nduru za juu za kisiasa, kidiplomasia na kijeshi za Ufaransa ziliratibu na kutekeleza mauaji hayo ya kimbari.

