Bukobawadau

SERIKALI WILAYANI NGARA KUANZA KUSAKA WANAFUZI WASIOKWEDA SHULE.

NGARA: Na Shaaban Ndyamukama, DATE.:April 4, 2014
 SERIKALI wilayani Ngara mkoani Kagera imewataka wakuu wa shule za sekondari wilayani humo kupeleka majina ya wanafunzi ambao hawajaripoti kuanza  kidato cha kwanza kwa maafisa watendaji wa kata ili hatua zichukuliwe kwa wazazi  wa wanafunzi hao
 Mkuu wa wilaya ya Ngara  Costantine Kanyasu amesema hayo leo wakati akiongea na maafisa watendaji wa tarafa na kata  kwenye ofisi yake na kudai kuwa muda wa kupeleka watoto shule kwa hiari umeisha tangu machi 31 mwaka huu
Kanyasu amesema kuwa wazazi pia wanatakiwa kuwapeleka shuleni wanafunzi hao kwa kukamilisha ada ya shule  vinginevyo katika kuondoa usumbufu wazazi watataifishwa mali zao ili wanafunzi wapate haki ya elimu
 “Tumetoa nafasi ya wazazi kupeleka watoto wao shuleni kwa hiari kulingana na baadhi yao kutegemea kuvuna mazao na  sasa wanauza badala ya kuwekeza kielimu wanatumia fedha kwenye ulevi sasa hivi ni msako” Alisema Kanyasu
Amesema kuwa katika wanafunzi 2, 770  waliofaulu katika shule 119 za serikali na binafsi wilayani humo kufikia Machi 31mwaka huu  ni 70% ya wanafunzi hao ndio wamewasili kwenye shule walizopangiwa na kuanza masomo yao.
 Aidha amesema viongozi watakaoshindwa kutumia madaraka waliyopewa kutekeleza maagizo ya serikali basi wajiandae kupoteza nafasi zao kwa kuvuliwa nyadhifa zao kwani serikali imechoka kubembeleza katika utendaji wa umma.
Next Post Previous Post
Bukobawadau