Bukobawadau

MH.MASSAWE MGENI RASMI KATKA KONGAMANO LA MAENDELEO 'BUGANGUZI DAY 2014' LILILOFANYIKA LEO APRILI 19,2014 BUGANGUZI WILAYANI MULEBA

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.Kanali mstaafu Fabian I. Massawe akiongea na Wananchi wa Kata ya Buganguzi Wilayani Muleba wakati wa Kongamano la maendeleo 'BUGANGUZI DAY 2014' lililoandaliwa na  BUGADEA.(Buganguzi Development Association)
 Mh. Massawe akizungumza na wananchi wa Buganguzi amewapongeza sana  wakazi wa Buganguzi walioko nje ya mkoa  chini ya mwavuli wa BUGADEA kwa kuwa na wazo la kukumbuka nyumbani na kushiriki kuchangia maendeleo.
 Mh. Massawe aliwapa changamoto wakazi wa  Buganguzi walioko ndani kutoa ushirikiano mkubwa kwa BUGADEA kwa kushiriki kuchangia chochote wanachoweza ikiwemo fedha, mali na nguvu kazi.  Alisisitiza  kuwa maendeleo ya Buganguzi yataletwa na wanabuganguzi wenyewe. Aliwahimiza wanaBuganguzi walioko nje ya Buganguzi na hata nje ya nchi kuja kuwekeza nyumbani  ili kuleta maendeleo. 
 Kushoto ni Ndg Lwamulaza ambaye ni (DMO) Wilaya ya Muleba,katikati ni Ndugu Roderick Lutembeka ambaye ni Mwenyekiti wa BUGADEA.(Buganguzi Development Association)wa mwisho ni Mh. Onesmo Yegira  Diwani wa Kata Buganguzi
SHILINGI milioni 8.8 zimekusanywa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Buganguzi, wilayani Muleba iliyoratibiwa na Umoja wa Maendeleo ya Buganguzi (Bugadea).
Akizungumza katika harambee hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa umoja huo ulioasisiwa na wakazi wa Kata ya Buganguzi waishio Dar es Salaam, Rodrick Lutembeka, alisema kiasi hicho kilitokana na michango ya wananchi, pia ofisi  ya mkuu wa mkoa imechangia  sh milioni 1.8 na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba imeahidi kuchangia sh milioni 30.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo iliyofanyika kwenye makao makuu ya kata hiyo, amehimiza wakazi mkoani humo kuepuka tabia ya kusubiri misaada na badala yake  wachangie miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Alisema juhudi za wananchi lazima zionekane kwanza katika miradi yao kabla ya kuomba misaada.
Alisema ni aibu kuomba misaada kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali hata kwa vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wa wananchi.
Massawe alisema miradi mingi ya maendeleo katika Wilaya  ya Muleba ukiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, haikutekelezwa kwa kasi ya kuridhisha kwa kile alichodai ni wananchi kurubuniwa na kushindwa kuchangia nguvu zao.
Katika kuhamasisha ujenzi wa Kituo cha Afya Buganguzi kinachokadiriwa kugharimu zaidi ya sh milioni 600,  Mkuu wa Mkoa ameshauri kila kaya kuchangia sh 20,000 au vitu vyenye thamani hiyo, ili kufikia lengo la kata hiyo kuwa na huduma hiyo.
Alipongeza wakazi wa Buganguzi walioko nje ya mkoa  chini ya mwavuli wa Bugadea kwa kuwa na wazo la kukumbuka nyumbani na kushiriki kuchangia maendeleo. Kata ya Buganguzi iliyo katika Tarafa ya Nshamba, ina vijiji vya Buhanga, Bushemba, Katare na Kashozi.
Mwenyekiti wa Bugadea, Lutembeka, alihimiza wakazi wa kata hiyo kuunganisha nguvu katika ujenzi wa kituo hicho na miradi mingine ya maendeleo.
Alisema hakuna sababu  ya kushindwa kufanya hivyo kwa kuwa fursa zilizopo,  ikiwemo ardhi na rasilimali  vinatosheleza kutekeleza ujenzi huo.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Rembris Kipuyo, alisema serikali itaendelea kushirikiana na wananchi wa kata hiyo hadi kukamilika kwa kituo hicho.
Diwani wa Buganguzi, Onesmo Yegira alipongeza uamuzi wa Bugadea kuandaa tamasha hilo la maendeleo lililopambwa na burudani pamoja na michezo mbalimbali ikiwa ni njia ya kukutanisha wakazi kuchangia maendeleo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbatama wakiimba wimbo wa maendeleo wa Mkoa wa Kagera.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mbatana akiongoza Wimbo wa Amani na Maendeleo.
Taswira mbalimbali wakati kongamano la BUGANGUZI DAY 2014 likiendelea
 Ndugu Roderick Lutembeka ambaye ni Mwenyekiti wa BUGADEA.(Buganguzi Development Association) akizungumza na  mwandishi wa Bukobawadau ,Mwenyekiti wa taasisi  isiyo ya kiserikali  BUGADEA(Buganguzi Development Association)ambayo inaratibu sherehe za Buganguzi day  kila mwaka amesema kauli mbiu ya 'BUGANGUZI DAY 2014' ni "BUGANGUZI KITUO CHA AFYA INAWEZEKANA NA WAWEZESHAJI NI SISI WENYEWE". Kauli mbiu hii inalenga kuwahamasisha wananchi kuendelea kuchangia kituo cha afya  bila kukata tamaa,Kituo ambacho kwa sasa tayari kipo kwenye ngazi ya msingi na kinakisiwa  kugharimu si chini ya shilingi milioni  mia sita (600,000,000).
Sehemu ya Wazee wa Kijiji cha Buganguzi wakimsikiliza mwenyekiti wa BUGADEA
 Akiongea na Wananchi wa Buganguzi Ndugu Ndugu Roderick Lutembeka amesema;Malengo yao bado  yanaamini kuwa sisi ni jamii tunayoweza kushirikiana katika masuala mengi yanayohusu maendeleo yetu.Kukutana pamoja kunalenga kutupatia nafasi  kuona namna tunavyoweza kuchangia jitihada za Serikali katika kukabiliana na changamoto za maendeleo ya mikoa yetu na wananchi wake.
 Wananchi wakiendelea kumsikiliza Ndg Mwenyekiti wa BUGADEA.(Buganguzi Development Association)
Mdau mwanakijiji Ndg Mzee.
 Afisa maendeleo Wilaya Muleba Bi Vavunge Oliver.
 Kushoto ni Mdau Mama Blandina, kulia ni Mzee Amry wa Buhanga Buganguzi.
 Sehemu ya wanafunzi.
Ndugu Alex Mtiganzi Mdau BUGADEA akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.Kanali mstaafu Fabian I. Massawe kufuatia maswala mbalimbali yaliyojili toka alfajiri ya leo  ikiwa ni pamoja na mashindano ya kukimia umbali wa Km 36 na kumuomba Mh. Mkuu wa Mkoa aweze kukabidhi zawadi kwa washidi waliopatikana.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.Kanali mstaafu Fabian I. Massawe akimkabidhi zawadi Mshindi wa kwanza  mwaka huu upande wa Wasichana mwanadada Aglipina Joseph Mtiganzi Zawadi ya Tsh 200,000 ikikabidhiwa kwa aliyeibuka mshindi wa kwanza kwa wasichana.
 Katika shangwe Baba Mzazi akimpongeza mwanae.
 Mwanadada Enelitha Kyaruzi,Mshindi wa pili  kutoka kijiji cha Katare Buganguzi anajinyakulia kitita cha Tsh.100,000
Enelitha Kyaruzi Akipongezwa na Mkuu wa wilaya wa Muleba.
 Mhe. Fabian  Massawe akitoa akitoa neno kidogo, kabla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi wa tatu  mwaka huu upande wa Wasichana.
Kwa jina anaitwa Sada Badlu, mshindi wa tatu  katika mashindano ya kukimbia umbali wa km 36 ,kituo cha kwanza ilikuwa Mbango shule ya Msingi ,Rutenge kamachumu Ijumbi Rubya, kishanda na mwisho mpaka Mbango-Buganguzi.
 Mshindi wa kwanza upande wa wavulana anaitwa Linus Emanuel anajipatia kitita cha Tsh.200,oo0
 Harakati za matukio zikiendelea.
Mshindi wa pili upande wa Wavulana anapata Tsh 100,000 ni Kijana Shubra Eliman.
 Mshindi wa tatu anaitwa  Dickson Peter.
 Ndugu Dickson akisaliana na meza Kuu.
 Wadau mbalimbali wanamaendeleo Kushoto ni Mzee Marios,katikati ni Mdau Jackson wa mwisho ni Ndugu Mwesigwa.
Mwenyekiti kijiji cha Bushemba Buganguzi
Lisala kwa Mkuu wa Mkoa kutoka chama cha wafanyakazi wastaafu kijiji Buganguzi
 Ndg Mwenyekiti na Mh Diwani Onesmo Yegila wakionyesha kuguswa na lisala hii
Mkuu wa Wilaya Muleba Mh. Lembris Kipuyo akiipitia lisala muda mchache baada ya kukabidhiwa nakala.
 Bi Methodia Peter akisalimiana na Mgeni Rasmi Mh. Massawe
 Jengo la Zahanati ya kata Buganguzi
Vyama mbalimba vya wanakijiji viliweza kuwakilisha mchango wa kuchngia Kituo cha  huduma ya Afya
Baada ya Mchakato mzima, Mwenyekiti wa (BUGADEA)Ndugu Roderick Lutembeka  anapata fulsa nyingine ya kutoa neno na  shukrani kwa Mkuu wa Mkoa pia  Takwimu kutokana na kilichopatikana kwa siku ya leo,akiongea na wananchi waliohudhuria kongamano hili na kuwaeleza kuwa historia inavyo onyesha toka mwaka 2011 ,BUGADEA waliadhimia kuwa kila mwaka wataendelea kuandaa matukio ya kuwaleta pamoja wana Buganguzi waliopo ndani na nje ya Mkoa wetu, Kiasi kilicho changwa ni 8,825,100M ambapo ofisi ya Mkuu wa Mkoa imechangia 1.8M
Kutoka Serikalini Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ameahidi  pesa ikipatikana atatoa 30M.
 Mdau Mama Muhazi
Kulia ni Fr. Gosbart.
 Wanaonekana Mama Muhazi na Mdau Alex Mtiganzi wakifurahia kilichopatikana kwa siku ya leo.
 Mwanakati Ndugu Mjumbe
 Mwendeshaji wa shughuli hii pichani ni Mtendaji Kata Buganguzi
PICHA ZAIDI YA 200 ZINAPATIKANA KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK,TAFUTA 'BUKOBAWADAU INTERTAINMENT MEDIA,
  VIDEO ZINAPATIKANA HAPA BUKOBAWADAU BLOG ZIPO ZIPO UKURASA WA MWANZO JUU YA HABARI HII!!
 'BUGANGUZI DAY 2014' ni "BUGANGUZI KITUO CHA AFYA INAWEZEKANA NA WAWEZESHAJI NI SISI WENYEWE'

Next Post Previous Post
Bukobawadau