Bukobawadau

WASANII WENGI WA TANZANIA WAMEPATA BAHATI YA KUCHAGULIWA KUSHIRIKI MAONYESHO MAKUBWA 2014,GERMANY

 Ngoma Ya Baikoko  kutoka Tanga Kutingisha  Jukwaa Ujerumani !
 FFU wa Ngoma Africa Band kama Kawaida Kukaza buti na mwendo wa kasi !
Mwanamuziki Jhikoman & Afrikabisa band kupeperusha bendera Tubingen !
Habari zipenya katika vianzo kuwa wasanii wengi wa Tanzania wanatarajiwa
kufunika katika maonysho makubwa mbali mbali nchini Ujerumani katika msimu wa joto.
baadhi ya wanamuziki waliopata bahati ni pamoja na kikundi cha ngoma ya Baikoko kutoka mkoani Tanga.
Wengine ni mwanamuziki nguli wa reggae Jhikoman & Afrikabisa band kutoka Bagamoyo mkoa Pwani ambaye amealikwa rasmi na Afrikative Organization
kushiriki onyesho kubwa la International Africa Festival Tubingen 2014 yanayo anza 17 mpaka 20 julai 2014 huko Tubingen,Ujerumani.

Wazee wa kazi Ngoma Africa band aka FFU aka Anunnaki elien,ukipenda waite "Watoto wa Mbwa" bendi isiyo ishiwa na habari inayoongizwa na kamanda mkuu FFU Ras Makunja wao kama kawaida yao kila mwaka wanajikuta wakiwa na kazi moja tu ya kupeleka mashambulizi katika kila jukwaa kuhakikisha washabiki wao wanaokadiliwa idadi ya milioni 50 duniani wapati usingizi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau