Bukobawadau

BIRTHDAY PARTY YA BI RUKIA KASSIM MAYENYA, MMEWE AFANYA KUFURU!!

Kubali au kataa, Mr &Mrs Abdulrahim (Simba) Mawenya ni miongoni mwa wanandoa  wenye majina makubwa Mjini hapa,Pia Mr  Abdulrahim (Simba) ni  mmoja wa Wadau wenye wake warembo na ni mmoja kati ya watu maarufu wenye msukumo mkubwa Mkoani Kagera na  maeneo ya Jirani,Haipiti wiki hajamtaja kwenye ukurasa wake wa Facebook na hakika kwa urembo wa Bi Rukia Kassim Mawenya,Ndugu yetu Simba maarufu kama  mzee wa Voda  ana haki ya kudata.
 Usiku wa Jana ilikuwa ni birthday ya mke wake huyo aliyezaa naye watoto wawili  na aliamua kumwangushia party ya nguvu iliyofanyika kwenye Kiota cha maraha  Linas Night Club Mjini hapa. 
 Muonekanowa Keki katika sherehe hii ambayo Bi Rukia anatimiza miaka kadhaa tangu aanze kuvuta hewa ya oksijeni.
Ikiwa ni siku maalum ya Bi Rukia Kassim, Unaweza kujionea kupitia Video yetu  iliyopo mwanzoni juu ya habari hii.
 “Happy birthday my darling wife Bi Rukia Kassim Mawenya. May you live to blow a million candles.
 Mr Simba anasema;''ukweli ni kwamba wewe ni zaidi ya kila kitu kwangu,tumetoka mbali na umekuwa ukinishauri na kunivumilia  katika mengi ya kimaisha,”
Nani hapendi kuwashiwa mishumaa, kula keki ya kuzaliwa na kupata zawadi nzuri juu ya siku yake ya kuzaliwa, Haya na mengine mengi usikose kucheck video ya tukio hili
 Kwa kuzingatia umuhimu zawadi ya Keki inatolewa
 Wadau pichani ni Elice Theobard na Modester Theobard.
 Wadau wakiwa wametulia tulii wakisubiri utalatibu
 Mr & Mrs Gilbart George(G-Smart)
 Mkurugenzi Mtensa, Mkurugenzi Bube wa LeoLeo na Mkurugenzi Peter Raphael Mugisha
Katika hali ya utulivu wadau wakibadilishana mawazo.
 Katikati ni Mdau Mohammed Kassim 'Kaka mdogo' wa Bi Rukia Kassim Mawenya.
Elizabeth (Nangai)Lweyendela na Bi Bena Deo wa Lugaibula
 Nancy Nafsa na Nancy Mollen
 Mwanadada Jesca Jess Jane kipata kumbukumbu ya picha dhidi ya wenzake

 Mwanadada Jesca pichani katikati na Mama Moha  Bi Rehena Gulam.


Kila Mdau anaonekana , kukoma kama sio kuchoka na Suprise  zinazoendelea ukumbini.
 Sehemu ya waalikwa wakisikilizia.
Kijana Ashmir na mwenzake Mkhusini,


Mdau Faustine Rutta wa Bukoba Sports, akifurahi na kinywaji  aina ya Climax kinacho chukua kasi kwa kizazi hiki,Climax ni kinywaji kisicho na kilevi, kilichotengenezwa na virutubisho kutokana na mimea asilia chenye ladha nzuri na kiongeza nguvu.
 Watu walivyo chomoka na kupendeza ukumbini
Shughuli ikiwa inaendelea ndani ya Linas Night Club, Kila kitu kipo sawasawa kabisa Waalikwa  tayari wameona na kuonja kile kilicho pelekea Mdau Abdulrahim Mawenya (Mr Simba) kumzuia mkewe  Bi Rukia  Kassim wa Mawenya asitumie fedha zake wala kuchangia chochote na kwamba kila kitu na gharama zote za juu zitakuwa juu yake na kweli imekuwa!!
 Ni fulsa kwa waalikwa kumpongeza Bi Rukia Kassim ikiwa leo ni siku yake ya kuzaliwa
 Pongezi kutoka kwa Waalikwa wote, zikiendela.
 Bi Nancy Nafsa na mwana  Dada DJ nikimaanisha Dyna James katika kumpongeza Rukia.
 Mdau Edgar na Mdau RMK Ramadhani Maulid Kambuga wao ni sehemu ya marafiki wa Bi Rukia.
 Mkurugenzi Mtensa,Mr Bube na Mkurugenzi Peter Mugisha.
Super Self Mkude akitetajambo na Mkurugenzi wa Linas Company & Linas Night Club.
 Swaggar za Bi Jesca Jess Jane
 Wadau  Katika hili na lile.
 Taswira mbalimbali ukumbini.
  Pichani ni sehemu ya Dada zetu,Shughuli hii na muonekano wa wageni wote  ukumbini hakika ni mfano wa kuigwa,watu wamevaa vizuri, wananukia,kuna baadhi wa wabishi humu Ukumbini wanaishi kama wapo mbele vile,namna wanavyojuwa kupangilia vitu,Kiufupi ni kwamba waalikwa walipendeza sana,BIG UP KWENU NYOTE mlio bahatika kuhudhuria Party hii.  
 Moja ya Picha kali ni wanadada Juliety Lyeyendela katikati wa Mwisho ni Hope wa Makoko
 Matukio zaidi yanapatikana katika Kurasa zetu za Facebook,ikiwa ni BUKOBAWADAU GROUP VIA facebook pia katika facebook page ijulikana kama Bukobawadau Entertainment Media
 Muendelezo wa matukio ya sherehe ya kuzaliwa Bi Rukia Kassim wa Mawenya.
Inadaiwa kuwa,kisa cha Ndugu Mrs Abdulrahim (Simba) Mawenya kuamua kumfanyia sherehe hii,Mkewe ni moja ya zawadi ya kumpenda kumtunza na kumvumilia kwa mambo mengi pia ni  kumbukumbu muhimu kama mshauri wa hatua aliyonayo kimaisha.
 Hii ndiyo zawadi ya Gari iliyotolewa,Gari ipo katika hali nzuri sana, inatumia Air spring,radio Car DVD Player GPS Navi bluetooth IPOD TV NAV-N7223 Nissan Murano ya mwaka 2011,kwa haraka haraka haya ndiyo niliyo yaelewa mie shuhuda wenu.
 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi akitoamaelezo kabla ya kukabidhi Faili la  Gari
Mr Bube akiwa mwenye furaha kutoa zawadi ya fedha taslim kwa Bi Rukia Kassim Mawenya kwa ajili ya mafuta ya Gari,ni sehemu  tu ya kusupport mizunguko ya hapa na pale.
Mdau  E. Nyamba ambaye amekuwa kimbilio la wengi kwenye mengi akitoleaj ambo ufafanuzi.
Kaka Mkuu E. Nyambo anakabidhi Faili la Gari ,na Mr Abdulrahim anakabidhi funguo pia.
 Zawadi nyingine ni Suti kali kwa Baba Mkwe wake
 Msanii Kamdingi akifanya yake katika Birthday Party ya Bi Rukia Mawenya.
 Mdau Prosper akionyesha kuguswa na Uimbaji wa Msanii Kamdingi wa hapa hapa Bukoba.
 Msani wa hapa Nyumbani Shemela akiwajibika kuupamba usiku wa Bday Party ya Bi Rukia Kassim wa Mawenya.
  Sehemu ya waalikwa wakisikilizia.
 Mdau John Do Pesa
 Mdau Mwinyi Kompyuta na Mkewe pembeni
 Salute kutoko kwa Mdau Rackson Kahabuka
 Zawadi kutoka umoja wa imara wa wanadada wa Mjini uliofungamana na kushikana mfano wa Nokia inavyowaka.
 Bi Lilian Peter Mwise rafiki wa karibu wa Bi Rukia Kassim Mawenya.
 Kaka Mkuu katika kuakikisha kila Mdau anapata huduma stahili.
 Mwanadada Jackline Erasmus
 Samsung Galaxy SIII ni moja kati ya Zawadi ambazo Ndugu Abdulrahim (Simba) Mawenya kamzawadia Mama Mkwe wake (Mama mzazi wa Bi Rukia)
 Wadau pichani ni Elice Theobard na Modester Theobard.
 Bi Jesca Jess Jane akikabidhi yake zawadi kwa Bi Rukia Kassim wa Mawenya.
Mh. Diwani Jeanifer Murungi Kichwabuta.
Mwanadada  Lorraine Nancy Mollen pichani kushoto na Bi Mahisara (Mama Kagutta)


 Mh. Matete akipata Nyama Choma.
 Meza ya Mdau AbdulRahym Kabyemela.
 Kaka Mkuu E. Nyambo akiendeleana  Shangwe Kabla ya kubwaga Manyanga
Kaka Mkubwa Ernest Nyambo ambaye hapo anasimama kama mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya shughuli hii,hakika jamaa huyu amekuwa kimbilio la wengi kwenye mengi,hapo akiwashukuru wadau waliojitokeza kwa wingi pia akiwaomba ushirikiano wa pamoja kwashughuli nyinezo kwani yeye anatangaza rasmi kujivua uenyekiti wa 'Pamoja Group'
 Kibengwe La Familia pichani ni Elice Theobard na Modester Theobard.
 Mama Mgole Shop na Mama Ruby.
Meza ya Kadanke G. Smart na Mdau Prosper.
 Tukio linalo endelea ni Wadau kupiga cheers na  Mr & Mr Mawenya
 Mama Rubby pichani
 Sasa ni mwendo wa Kadansee, Yelele...full BURUDANI.
 Kaka Mkuu Full kusebeneka!!
Bi Rukia Kassim Mawenya anatoa shukrani zake za dhati kwa mme  wake na kuwashukuru wadau wote waliohudhuria shughuli ya kuzaliwa kwake
  Hii ni moja ya Sherehe kali yenye SUPRISE mwanzo mwisho ,watu wamekua na furaha,watu wame kula na kunywa mpaka basiiiiiiii!! zawadi kemkem hadi kwa wazazi ,taswira yakuvutia waalikwa ukumbini ......Endelea kuwa nasi
Next Post Previous Post
Bukobawadau