Bukobawadau

MAKAMU WA RAIS AZINDUA RASMI MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA UWANJANI KAITABA MJINI BUKOBA LEO MAY 2,2014


 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal amezindua rasmi Sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba , Mkoani Kagera leo na kuwataka watanzania Bara na Zanzibar kudumisha umoja na amani iliyopo.
 Akizungumza na wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Kaitaba, Dkt. Bilal amesema Mwenge  wa Uhuru ni kielelezo cha Umoja wa Watanzania, kama ilivyo falsafa ya mbio za Mwenge kumulika mpaka nje ya mipaka na kuleta amani palipojaa dhalau na matumani.
 Walimu wakufunzi wa Chipukizi
 Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kuuwasha rasmi wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.  
Mkuu wa Mkoa waKagera Kanali Mstaafu, Fabian Massawe.
  Mkuu wa Mkoawa Kagera akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Vijana wenye dhamana ya kukimbiza mwenge wa Uhuru 2014, wakianza rasmi mbio hizo baada ya kuwashwa na kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
 Amesema mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa kielelezo na kuzingatia falsafa ambayo ndio dira, historia na alama ya Watanzania, jambo ambalo amedokeza kuwa viongozi na wananchi kwa ujumla wanawajibika kujikumbusha dhana ya Mwenge na Falsafa hiyo kwa kutafakari maneno ya busara yaliyotamkwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
 Sehemu yamaelfu ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa sherehe za Mbio za mwenge.
 Wadau pichani ,kamati yamapokezi.
 Pichani ni wageni waalikwa, kutoka serikali ya Japan

TUNATATIZO KUBWA LA KIMTANDAO NDUGU WASOMAJI,HABARI HII ITAENDELEA BADAE KWA PICHA ZAIDI, AUDIO NA VIDEO ZA HOTUBA MBALIMBALI

Next Post Previous Post
Bukobawadau