Bukobawadau

DC WA KARAGWE APATA AJALI

MKUU wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Darry Rwegasira amepata ajali katika Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Nyamirembe Wilayani Chato mkoani Geita juzi.
Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Said Magalula, alisema Rwegasira alipata ajali hiyo akiwa na gari namba STK 3768 akiwa safari kuelekea wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Magalula alisema chanzo cha ajali hiyo ni hatua ya dereva Said Adamu (59), kujaribu kumkwepa mtoto Jonas Tyson (7) ambaye alikatisha ghafla barabarani na kusababisha gari kupinduka na kuharibika vibaya.
Hata hivyo, katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha na hali za majeruhi akiwemo mkuu huyo wa wilaya zinaendelea vizuri.
Next Post Previous Post
Bukobawadau