Bukobawadau

IZIGO MULEBA-OMUKIGANDO,MUBUNDA NA CAMERA YETU LEO MAY,2014

Camera yetu Kijijini Izigo,eneo hili na eneo jirani la  Kata ya Muhutwe  na Kagoma katika Jimbo la Muleba Kaskazini tatizo la maji limezidi kuwa kubwa baada ya kukosekana kwa vyanzo vya uhakika  licha ya Kata hizo kupakana na Ziwa Victoria na Mto Ngono
Muonekano wa Center ya kuu ya Izigo ndani ya Wilaya Muleba,ambapo ni miaka kadhaa sasa,Halmashauri hii imeendelea na mchakato wa kumwajiri Mtaalam na wananchi kuhakiki vyanzo vya maji na kusanifu miradi ya maji katika vijiji kumi ambavyo ni Katoke, Iroba, Kiragi na Muyenje katika Jimbo la Muleba Kaskazini, vijiji vingine ni Katembe, Kishoju, Kangaza, Kyota, Kabale na Karutanga, Jul 26, 2013 tumeshuhudia Mh. Rais akizindua mradi mkubwa wa maji wilayani hapa.
Taswira eneo la Kagoma Wilayani Muleba,Sekta ya shughuli za uvuvi katika Ziwa Victoria pamoja na umuhimu wake bado haijasimamiwa kikamilifu, asilimia kubwa ya wadau uchumi wao umeshindwa  kuchangamka.
 Ndani ya Tarafa ya Izigo,kijiji cha Kabare ndipo ulipogundulika Ugonjwa wa Mnyauko kwa mara ya kwanza mwaka 2005 Mkoani Kagera, ugonjwa ulio ingia nchini Tanzania kutokea Uganda.
Soko la samaki wanaovuliwa kwa zana za kisasa-viwanda, kuna dalili za kuwepo njama miongoni mwa wenye viwanda kupanga bei ya samaki. Baya zaidi ni kuwa bei inayotolewa ni ndogo sana, haikidhi gharama za uzalishaji. Baya zaidi bei hiyo kwa Mwanza ni ndogo kuliko inayotolewa na wanunuzi toka Uganda na Kenya huko huko visiwani
 Tatizo la bei linapelekea samaki kununuliwa  na viwanda vya nchi jirani. Hatua hii kwa hesabu za haraka itaua viwanda vyetu, kuathiri ajira, kuikosesha Serikali yetu kodi na ushuru utokanao na shughuli za viwanda hivi vya ndani.
 Barabara kuu Wilaya ya Muleba ,mojawapo ya Wilaya kubwa sana Tanzania
 Moja ya kituo cha mafuta kilicho jengwa kisasa ndani ya Mji Mdogo wa Muleba.
Bukobawadau Blog moja kwa moja kutoka pande za Muleba.
Stend kuu ya Mabus Mjini Muleba.
Jengo la E.L.C.T lililopo Muleba.
 Njia panda kuelekea Biharamulo na Nshamba.
Taswira  Kijijini Omukigando, milima na mabonde Vijiji jirani vya Mubunda, Bulamula-Bukongo na Busheka Wilayani Muleba.
  Swala la huduma ya maji Wilayani Muleba bado ni changamoto
Camera yetu ndani ya Kijiji cha Kamishango Wilayani Muleba
Barabara kuu kuingia na kutoka vijiji vya  Nshamba; Kimeya – Mubunda – Kibanga – Kamishango - Ikondo – Luhanga.
 Muonekano wa Msikiti uliopo Omukigando
Eneo la makazi kijijini  Kamishango.
 Barabara kuelekea Tarafa za Kimwani na Nshamba.
Next Post Previous Post
Bukobawadau