Bukobawadau

TIMU YA MPIRA WA MIGUU KIKUKWE STARS YAFADHILIWA

 Timu ya mira wa miguu ya kijiji cha Kikukwe-Kikukwe Stars iliyotwaa kombe la Parokia katoliki ya Kanyigo
 Baadhi ya vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa.
Mfadhili wa Kikukwe Stars Johaness Mukayu(mwenye viatu vyeupe) akitoa nasaha zake
 Michezo,Missenyi NA MUTAYOBA ARBOGAST.
 Bw.Johaness Mukayu,aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kujipongeza kwa timu ya mpira wa miguu ya kijiji cha Kikukwe kata ya Kanyigo kwa kunyakua kombe la ligi ilyoandaliwa na parokia Katoliki ya Kanyigo mwezi Desemba mwaka jana ikizishirikisha timu tisa za kata ya Kanyigo na Kashenye ametoa zawadi kwa timu hiyo kama alivyoahidi.
Bw,Mukayu ambaye ni mzaliwa wa kijiji hicho na anafanya kazi katika shirika la Worldvision wilayani Muleba,jana aliikabidhi timu hiyo vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya sh.laki tano.
Vifaa hivyo ni jezi kwa wachezaji 16,soksi jozi 16,mipira miwili na kipenga.
Aliwataka wachezaji kuhubiri amani kwani pasipo amani hakuna shughuli ya maendeleo inayoweza kufanyika,na akawataka pia kudumisha maadili kwani wachezaji ni kioo cha jamii.
Timu hiyo ya Kikukwe Stars katika mchezo wa fainali iliilaza timu ya Super-Eagles ya kijiji cha Kigarama kwa magoli 2-1 na kubeba kombe pamoja na sh laki tatu taslimu huku mshindi wa pili alizawadiwa sh laki mbili.
Next Post Previous Post
Bukobawadau