Bukobawadau

AJALI MBAYA YATOKEA ASUBUHI YA LEO ENEO LA BUNAZI,WATU WAWILI WANUSULIKA KIFO!!

 Ajali hiyo imetokea majira ya saa 3:00 asubuhi ya leo June 9,2014  katika Kijiji cha Kabwela Kata ya Bunazi ,Wilayani Missenyi,Watu wawili wamenusulika kufa katika ajali hiyo, watu hao ni Mfanyabiashara  maarufu wa Mutukula ajulikanaye kama Mr Morgan akiwa na Afisa Uhamiajia anayejulikana kwa jina la Daudi Mwala.
 Mpaka jioni hii Majeruhi  wamelazwa katika hospital ya Mkoa iliyopo Mjini Bukoba

Gari aina ya  Toyota Harrier yenye nambari za Uganda UAT740D lilikuwa likitokea Kyaka  Mjini kuelekea Mutukula, limepoteza mwelekeo na kuacha njia kuu huku likiwa na mwendo mkali na kuelekea bondeni njia panda kuelekea kiwanda cha Sukari cha zamani Kagera A.

Next Post Previous Post
Bukobawadau