Bukobawadau

GERMANY 2-2 GHANA:Ni Asamoah Gyan Kabla ya Klose kusawazisha!!

Miroslav Klose akitokea benchi anaipatia Ujerumani bao lakusawazisha , ni mpira wa kwanza kuugusa baada ya kuingia tu  uwanjani ,Germany 2-2 Ghana.
Bao la Klose linamuweka kwenye historia ya kuweza kupata Magoli 15 kama Ronaldo kwenye historia ya michuano ya kombe la Dunia .
 Maumivu makubwa kwa kipa wa Ghana Fatau Dauda baada ya kufungwa  bao la pili na Ujerumani.

Kwa njia ya kichwacha mchezaji  Andre Ayew ndivyo anavyo onekana Kipa wa Ujerumani  Manuel Neuer akijaribu kuufuata mpira  bila mafanikio.Germany 1-1 GHANA (A Ayew 54)
 Ndivyo alivyo ruka juu zaidi Mchezaji Andre Ayew  na kuipatia Ghana hesabu ya bao la kwanza.
 Mario Gotze baada ya kuipatia Ujerumani bao la kwanza.
Nahodha wa Ghana Asamoah Gyan uso kwa uso na Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer .
Katika kuwajibika anaonekana Kipa wa Ghana, Fatawu Dauda  akijaribu kumzuia Thomas Muller .
 Katika kukabiliana na mtiti uwanjani ,anaonekana  nahodha wa Ujerumani Philipp Lahm na Christian Atsu pichani (kushoto)
 Katika picha anaonekana beki wa Germany Jerome Boateng akisalimiana  na Kaka yake, ambaye ni mchezaji wa Ghana Kevin-Prince Boateng .
 Mmoja wa shabiki wa ujerumani.
 Mashabiki wa Ghana wakiwa wamevalia vyema mavazi  yao yenye mng'ao, yenye kuvutia na kuwashangaza wenzetu .
Mashabiki wa Ujerumani Wakionyesha matumaini  kuwa Kombe la Dunia 2014 ni haki yao .
Taswira nje ya Uwanja,Sasa Ujerumani kukutana na Marekani katika mchezo wa mwisho Ghana uso kwa uso na Ureno.
Katika swala zima la kuweka pozi katika picha , ndivyo wanavyo onekana mashabiki mbele ya Camera ndani ya Uwanja wa Castelao Fortaleza .GERMANY 2-2 GHANA

Next Post Previous Post
Bukobawadau