SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

21 June 2014

WATU ZAIDI YA 10 WAPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA GARI ILIYOTOKEA ENEO LA MAKONGO JIJINI DAR MCHANA WA LEO JUNE 21,2014

 Watu zaidi ya kumi wamepoteza maisha kwenye ajali ya Daladala inayofanya safari zake kati ya Ubungo - Tegeta jijini Dar mchana huu,baada ya kushindwa maarifa ya kiudereva kwa Dereva wa daladala hilo hali iliyompelekea dereva huyo kuhama mpaka upande wa pili wa barabara na kulivaa lori kwa nyuma.Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa kuwa ni mwendo kasi.
   Tunaomba ladhi kwa picha zinazoendelea hapa chini, Zinatisha sana.
b  Hili ndilo lori lililokuwa likipita katika upande huo wa Barabara na kufatwa na daladala hiyo. 
 Tunaendelea kuwaomba radhi kwa picha hizi zinatisha.
 Ajali imetokea mchana wa Leo Jumamosi June 21,2014 Jijini Dar

2 comment:

Prudence Karugendo said...

Madreva wanatumaliza sisi tukiwa tunawaangalia tu! Wengi wa madreva ni wavuta bangi, wanaendesha magari kibangi bila sisi kutia neno, na ikitokea ukasema kuwa mwendo anaoenda dreva si wa usalama unaweza kushambuliwa na abiria wenzako kabla ya unayemlenga! Bila sisi wenyewe kujirudi hawa wavuta bangi watatumaliza.

Anonymous said...

ooooh God!!! Hivi hii hali kweli na .......... ukweli dada M/S. Prudence kaongea tayari. Natoa salam za pekee kwa ndugu na Jamaa walopoteza ndugu na pia kwa Taifa letu, ebu jamani tuangalie na vifo vingine basiiiiiiii aaahhh inaumaaa nyie!!! acha tu

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU