Bukobawadau

HISTORIA YA MAISHA YA MREMBO MILLEN MAGESE

HAPPYNES MILLEN MAGESE jina hili sio adimu sana masikioni mwa watanzania walio wengi,huyu ndiye aliyewahi kuwa miss Tanzania mwaka 2001 na kujizolea umaarufu wake hapa nchini na nje ya Tanzania.

     Pamoja na kuwa miss Tanzania mrembo huyu amebahatika kuwa na kipaji cha uwana mitindo kipaji ambacho kimempa mafanikio makubwa hata kumpa umaarufu wa dunia kwa shughuli hiyo ya uwanamitindo.

      Mrembo huyu baada ya kufanikiwa kuwa miss Tanzania alifanikiwa kuhamia nchini Africa ya kusini ambako alianza kufanya kazi zake za uwana mitindo na kujizolea umaarufu mkubwa sana na baadae kuishi pia nchini marekani kwa ajili ya kazi hiyo hiyo

    Historia ya binti  huyu ni kubwa sana kwani ni moja kati ya warembo wa Tanzania waliotumia vizuri nafasi walizopata kwa ajili ya kujiendeleza na kupata mafanikio
Kabla ya MILLEN kuwa miss Tanzania akiwa na umri wa miaka 15 tu alianza kupata tatizo ambalo lilikuwa linamkosesha raha sana tatizo ambalo kwa hapa Tanzania walishindwa kujua nini kinamsumbua hasa,kwani alikuwa akipata maumivu makali wakati wa hedhi kwa wale wanawake wanaelewa,na pia alikuwa hana muda ama kipindi maalum cha kuingia katika hedhi muda wowote alikuwa anaweza kuingia na kupata maumivu makali sana.
Baadhi  ya wanafunzi ambao pia wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo wakiwa katika semina hiyo iliyoandaliwa na mrembo MILLEN MAGESE wikiend hii jijini dar es salaam
MILLEN MAGESE anapokumbuka mateso aliyopitia haachi kulia hata mbele za watu kwa inauma sana,katika semina hii alimwaga chozi
 Tatizo hilo lilimsumbua kwa takribani miaka yote ambayo aliyokuwa nchini na madaktari nchini walishindwa kujua nini hasa kunamsumbua.MILLEN baada ya kwenda kuishi Africa ya kusini tatizo hilo lilizidi sana na kuamua kuwaona wataalam mbalimbali nchini humo kwa ajili ya vipimo  ambapo walifanikiwa kujua ni tatizo gani lilimpata.

   ENDOMETRIOSISI ni ugonjwa ambapo ni mgeni sana masikioni mwa watanzania ambapo hata kishwahili chake bado hakijapatikana ni ugonjwa ambao humsababishia mgonjwa maumivu makali sana kipindi cha hedhi na husababisha pia mgonjwa kutopata mtoto.

   Huu ndio ugonjwa uliomkuta mrembo MILLEN MAGESE ambapo ilibidi afanyiwe upasuaji wa kizazi kwa mara 12 nchini Africa ya kusini kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo jambo ambalo linasikitisha sana.
akitoa semina 
  “Nimefanyiwa upasuaji wa kizazi mara 12 nchini Africa ya kusini kwa msaada wa marafiki zangu ili kuokoa maisha yangu,sina uwezo wa kupata mtoto tena mirija yangu yote imeziba na madactari wanasema haiwezi kuzibuka tena”aliiambia habari24.

  Mrembo huyo kwa sasa yupo nchini na HABARI24 BLOG imefanikiwa kukutana naye na kufanya naye mahojiano maalum ambapo ametueleza lengo lake la kurudi nchini Tanzania

 “Nimekuja Tanzania sasa kwa lengo moja kuwaokoa watanzania na kuwajengea uelewa juu ya ugonjwa huu  chini ya mpango wangu wa MILLEN MAGESE FOUNDATION ,kwa sababau ugonjwa huu kwa hapa Tanzania unaonekana bado haufahamiki japo watu wengi sana unawasumbua kiasi kwamba wanakosa raha maishani na kikubwa zaidi hakuna hata kipimo cha ugonjwa huo hapa nchini Tanzania”aliiambia HABARI24 BLOG
 Kwa kuanza na hilo la kuwaelimisha watanzania wikiend hii mtandao huu ulimshughudia mrembo MILLEN akiwa anatoa semina kwa wanafunzi,kina mama na watanzania zaidi ya mia moja juu ya ugonjwa huu ambapo walimshukuru sana kwa huduma hii.

  Katika maongezi yake MILLEN ameigeukia serikali na kuiomba kuhakikisha unawasaidia wagonjwa wa ENDOMETRIOSIS ikiwa ni pamoja na kuwajengea hospitali maalum ya ugonjwa huo 
USIKOSE HAPA HAPA TUTAKUPA USIKIE SAUTI YAKE AKIZUNGUMZA NASI
  

Next Post Previous Post
Bukobawadau