Arsenal huenda wakamkosa kipa wa Real Madrid, Iker Casillas, baada ya
mpenzi wake kudai kuwa hatohama kutoka mji mkuu wa Spain, Madrid (Daily
Express),lakini Arsenal huenda wakamsajili mshambuliaji wa Real Madrid
Alvaro Morata na wapo tayari kupambana na Tottenham na Inter Milan
wanaomtaka pia (Daily Express).
Barcelona wamefikia makubaliano yasiyo
rasmi na Marcus Reus wa Borussia
Dortmund. Reus amekuwa akifuatiliwa pia na Manchester United
(Talksport), wakati huohuo Manchester United wapo tayari kupokea pauni
milioni 12 kwa kiungo wake Marouanne Fellaini ambaye alisaini mwaka jana
kutoka Everton kwa pauni milioni 27 (Daily Star), Chelsea wanajaribu
kumsajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona katika mkataba ambao
utahakikisha Arsenal haipati nusu ya faida itakayopata Barcelona (Daily
Telegraph), Pepe Reina atarejea Liverpool kwa kuwa Napoli inashindwa
kufikia madai ya Liverpool ya kubadili mkataba wa mkopo kuwa wa moja kwa
moja (Metro), Manchester City watakamilisha usajili wa beki wa kati
kutoka Porto, Fernando ifikapo mwisho wa wiki hii na pia kukamilisha
usajili wa Bacary Sagna kutoka Arsenal(Daily Mail), Everton wana tumaini
watafanikiwa kupambana na Arsenal katika kumsajili Samuel Eto'o kutoka
Chelsea (Daily Express).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment