Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Jennifer Lopez amebadili msimammo wa
kutohudhuria sherehe za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia, na
kutangaza kuwa atakuwa sehemu ya sherehe hizo zitakazofanyika kesho huko
Arena de São Paulo, mjini São Paulo.
J-Lo ambae hakutoa sababu za kutohudhuria sherehe hizo siku mbili
zilizopita, amesema ameona kuna umuhimu wa kuhudhuria katika sherehe za
ufunguzi hivyo hii leo usiku anatarajia kusafiri kuelekea nchini
Brazil.
.Amesema anaamini mashabiki wake walisikitishwa na taarifa ambazo
zilitolewa na shirikisho la soka dunia FIFA za kutokuwa sehemu ya
sherehe hizo hapo kesho, hivyo ameona sio jambo jema kufanya hivyo kwa
kuhisi huenda akawanyima haki wanaompenda kumuona akiwa jukwaani
sambamba na wasanii wengine, ambapo wataimba wimbo maalum wa kombe la
dunia wa mwaka huu unaoitwa ‘We Are One’
Wasanii wengine watakaoshirikiana na Jennifer Lopez kuimba wimbo huo ni Pitbull na mwenyeji Claudia Leitte.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment