Bukobawadau

MARADONA AWABWATUKIA FIFA KWA KUIKOSEA HESHIMA COSTA RICA.

Nguli wa soka duniani na mkali wa enzi hizo wa Argentina, Diego Armando Maradona, amewafananisha viongozi wa FIFA na genge fulani la wahuni lisilo na nidhamu wala heshima, kufuatia hatua ya shirikisho hilo la vyama vya soka duniani, kuamuru kuchukuliwa mkojo kwa wachezaji saba wa timu ya taifa ya Costa Rica, waliokuwa uwanjani siku timu hiyo ilipoibamiza Italia kwa bao 1-0 na kufuzu kwa hatua ya 16 bora.
Maradona, anaamini kuwa kitendo cha FIFA kutaka kupima mkojo wa wachezaji hao kuwa walitumia dawa za kuongeza nguvu au laa, ni cha kudharau mabadiliko chanya makubwa ambayo Costa Rica wameyafanya katika mfumo wao wa soka, mabadiliko ambayo ndio yamewapa mafanikio waliyofikia hadi sasa katika Kombe la Dunia.
VIA Jukwaa Huru Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau