Bukobawadau

WANAWAKE,VIJANA WILAYANI MULEBA WATANGEWA MIL.69/-

HALMASHAURI ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagara, imetenga zaidi ya sh milioni  69 kwa kipindi cha mwaka 2010/2014 kwa ajili ya mikopo kwa vyama vya akiba na mikopo (Saccos) vya kinamama na vijana, ili kuwawezesha kukopa na kujiajiri.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mkuu wa Wilaya, Lembris Kipuyo, katika taarifa yake aliyoisoma kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfley Zambi  alipokuwa ziarani mkoani Kagera.
Alisema wilaya hiyo imeendelea kuviwezesha vikundi vya kinamama na vijana kwa kipindi hicho chote  kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu, ili wakope, wazalishe na kujijengea uwezo kiuchumi na hatimaye waondokane na umasikini wa kipato.
Kipuyo alisema mbali na mikopo hiyo, halmashauri  ilitoa sh milioni 9 kwa ajili ya mafunzo kwa vijana wapatao 15 na kununua mashine saba za kufyatua matofali ya gharama nafuu kwa kutumia udongo na saruji kidogo.
Alisema mpango huo unaanza kutekelezwa katika kata tano za wilaya hiyo ambapo vikundi vitano vyenye washiriki 50 vimenufaika na mpango huo.
Pia alisema vijana wapatao 176 wamepata mafunzo ya ujenzi wa nyumba bora za bei nafuu kutoka kwa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Vifaa vya Ujenzi wa Nyumba Bora.
Alieleza kuwa vikundi 19 vya watu wanaoishi na VVU/Ukimwi vyenye jumla ya wanachama 1,089 vimeundwa na kupewa msaada wa mbuzi wa maziwa 123, chakula na huduma ya malazi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau