Bukobawadau

ENGLAND WANAREJEA KWAO NA POINT MOJA;England 0-0 Costa Rica World Cup 2014

Kiungo na nahodha wa England Steven Gerrard pichani  (katikati) akipasha na wenzake.

Mtazamo tofauti kwa mmoja wa mashabiki wa Uingereza
Inaonekana Kivutio pale mashabiki wa Brazil wanapo ingia Uwanjani Belo Horizonte kuangalia  mchezo kati ya England na  Costa Rica .
Mashabiki wa Uingereza wakizungusha Bango jukwaani lenye ujumbe kwaPrince Harry .
Aliyesimama katikati ni Prince Harry  muda mchache kabla ya mtanange kuanza ndani ya uwanja wa Estadio Mineirao kati ya  England wakichuana na Costa Rica .
Mchezaji Joel Campbell pichani (kulia) wa Costa Rica akiambaa na mpira mbele ya udhibiti wa Adam Lallana
Ni mchezaji Mdogo na hatari Ross Barkley pichani (kushoto) wa Uingereza akimdhibiti  Yeltsin Tejeda ya Costa Rica 
La familia pichani ni mke wa Mchezaji  Wayne Rooney , Colleen akimwangalia mtoto wao Kai jinsi alivyo makini na ufuatiliaji wa mpira uwanjani.
Hakuna penati hapa ni baada ya Mchezaji  wa Uingereza  Daniel Sturridge (kushoto) kuchezewa vibaya na Mchezaji  Oscar Duarte wa Costa Rica
 Anaonyesha ukakamavu mchezaji Jack Wilshere wa England akikataa kutoa njia kwa na kuudhibiti mpira dhidi wa Oscar Duarte ya Costa Rica 
Kipa wa England Ben Foster anaruka kuokoa mpira wa hatari.
Mchezaji Frank Lampard wa England anaonekana kumudu na kudhibiti  nafasi ya kiungo mwanzoni mwa kipindi cha kwanza. 
Wanachekelea mashabiki wa Uingereza kuhusu kutolewa kwao mapema
Ndugu umenionea, ndivyo anavyo onekana Mchezaji Jack Wilshere wa England akimlalamikia mwamuzi Djamel Haimoudi dhidi ya maamuzi aliyotoa dhidi yake. Full- time England 0-0 Costa Rica World Cup 2014
Anafanya kuokoa Kipa Keylor Navas wa Costa Rica ilikuwa nafasi kwa Daniel Sturridge.
Amekosa nafasi ya wazi Mchezaji wa  England Daniel Sturridge kama anavyo onekana akishika kichwa.
 Hali ishakuwa ndivyo sivyo uwanjani , kwa gharama yoyote ndivyo anavyo zuiwaMchezaji wa Uingereza Ross Barkley pichani (kulia) kwa kufanyiwa madhambi na  Giancarlo Gonzalez wa Costa Rica
Kwa matokeo haya England inaondolewa Rasmi katika michuano hii, Sijui anamaanisha nini kocha  wao Roy Hodgson kwa  ishara hii.
 Polisi wanaingilia kati kutuliza hali ya mvutano iliyojitokaza kati ya mashabiki wa Uingereza na Brazil.

Next Post Previous Post
Bukobawadau