Fanya kupitia Stori hii inayomhusu jamaa pichani kushoto.
Kuna incident imetokea maeneo ya sinza naomba niwarushie kama ilivyo ili tujifunze kitu
leo asubuhi wamekuja watu 6nyumbani wakasema wanatoka tanesco
wamekuja kucheki mita ya luku.wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa
hiyo wanakata umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye gps yao kuwa
umeme hauendi vema.macho yakatutoka,wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi
ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia.nikawauliza kama
mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwa mwezi?si ingepaswa
tulipe kidogo?wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo
kifaa cha kuiba umeme) huwa kinafyatuka halaf umeme unakwenda zaidi!
wakakata umeme
wakaondoka,tujipange.tujadiliana na mzee tukapata mashaka
maana walikuwa wakali halaf wanalazimisha mambo,wamevaa vitambulisho
lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki.tukapiga simu tanesco kuwauliza
wakasema hao ni vishoka tuite polisi.basi tukawapigia simu waje wachukue
laki tano waturudishie umeme,mengine j3. wakaja fasta2 wakarudisha
umeme.nikawaambia naenda ATM wasubiri.nikawaacha na mzee.nikatoka mbio
mpaka polisi chuo nikawahadithia wakanipa polisi 3 nikaja nao
home,tukawakuta wameondoka.mzee akawapigia simu waje hela
imepatikana.wakasema tukutane mlimani city,tukafanikiwa kukamata mmoja
wengine wakakimbia.tumemuacha selo,tukaandikisha maelezo.tunasubiri
hatua itakayofuata.hiyo picha ndo huyo tuliyemkamata! NDUGU WADAU KUWENI MAKINI NA UTAPELI WA AINA HII!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment