Bukobawadau

FULL-TIME; BARAZIL 2-1 COLOMBIA; David Luiz anawapeleka Wenyeji hatua ya Nusu Fainali

Mashabiki wa Brazil wakiwa wamebeba bango la Mick Jagger ikiwa ni utani kwa Colombia.
Wanaonekana mashabiki wa Brazil
Mapema kabla ya mchezo ,shabiki wa Brazili anatabili matokeo ya 2-1 na kweli ndivyo inavyokuwa.
Mpiga picha anajipatia Busu la upendo  kutoka kwa shabiki wa Brazil ndani ya uwanja Estadio Castelao.
Ndivyo alivyo onekana Mchezaji  Neymar wakati wanawasili uwanjani
Mchezaji Hulk wa  Brazil akiwasili uwanjani
Anaonekana Mchezaji David Luiz akisikiliza muziki wakati anaingia uwanjani
Wanaonekana mashabiki wa Brazil kabla ya mechi kuanza ndani ya Uwanja wa Estadio Castelao 
Pwani ya fukwe za Capacabana sehemu yenye raha na vibweka vya kila aina  anaonekana mwanamke shabiki wa Brazil akijiachia kana kwamba tayari matokeo anayo.
Muonekana chumba cha kubadirishia cha wachezaji wa Brazil  
Taswira uwanjani.
Ni Sanamu la Mchezaji Hulk wa Brazil likiwa limeinuliwa na mmoja wamashabi muda mchache  kabla ya mchezo wa Robo fainali ya Kombe la Dunia 2014  
Muda mchache kabla ya kuyakabili majukumu uwanjani wanaonekana Mchezaji Neymar (kushoto)na Hulk. 
Kutuma ujumbe: Wachezaji Colombia na Brazil Wanasima,a nyuma ya bango la  FIFAlenye ujumbe wa kupinga ubaguzi wa rangi. 
 Mfungaji wa bao la kwanza la Brazil,Thiago Silva anapata wakati mgumu kutoka kwa mchezaji wa  Colombia Victor Ibarbo
David Luiz akionyeshana umwamba na Mchezaji wa Colombia Mario Yepes 

Neymar anashindwa kuzuia mpira na kupalaza katika kichwa chake
 Mshambuliaji wa Brazil  Fred pichani (kulia) akilalamika baada ya kuchezewa vibaya na Mchezaji wa Colombia Carlos Sanchez 
 Wachezaji wa Colombia wanapoteza umakini baada ya mpira wa kona ,Unaomkuta  Mchezaji Thiago Silva ,Naye anafanya kitendo laisi sawa na kumsukuma kiwete vile na kuandika gole kwa kwanza kwa Brazil.
 Beki na nahodha wa Brazil Thiago Silva (kulia)na kiungo Paulinho wakishangilia bao lililopatikana mwanzoni mnano dakika ya 7 ya mchezo
Shangwe za Goli! BRAZIL 1-0 Colombia
 Mchezaji Neymar (kushoto) akiwa ameanguka wakati wakishangilia bao la kwanza la kuongoza.
Kwa uchungu mkubwa kwa ajili ya Timu yake ndivyo anavyo onekana Mchezaji wa Brazil David Luiz katika moja ya changamoto dhidi ya Mchezaji Teofilo Gutierrez wa Colombia 
 Ni hatari lakini salama anaweka Mguu wake Mchezaji wa  Brazil Fernandinho (kushoto)kumzuia mchezaji wa Colombia  James Rodriguez 
Vita uwanjani ni Mchezaji wa Brazil Fernandinho (kushoto)akikabiliana  na Fredy Guarin wa Colombi 
Anaonekana kifua mbele ni Beki wa Brazil i Brazil Luiz David akishangilia baada ya kufunga bao la pili kwa timu yake.
  Bila mafanikio anaonekana Kipa wa Colombia David Ospina akifuata mpira , ni Goli la pili la Brazil lililofungwa na Beki mwenye swagar David Luiz 
 Luiz anaruka juu na kupiga teke kibendera ikiwa ni furaha ya bao la pili la ushindi
 David Luiz katika furaha yake
David Luiz akishangilia sambamba na kelele za maelfu ya mashabiki uwanjani
Mashabiki na wachezaji wakishangilia bao
 Colombia wanapata penati na Mchezaji James Rodriguez anafanya kweli.GOAL! Brazil 2-1 COLOMBIA
 Ikiwa ni dakika ya 80 Mchezaji kiungo wa ColombiaJames Rodriguez anashangilia bao lake lililopatikana kwa njia ya penati
Chini ni Mchezaji  Neymar wa Brazil , kulia ni mchezaji mwenzake Marcelo akiomba msaada kutoka kutoka katika benchi la ushindi 
Mpaka hapa Bukobawadau Blog, hatuna la ziada  usikose kuwa nasi kesho katika michezo mingine ya hatua ya robo fainali ya Kombe la dunia kati ya  Uholanzi na Costa Rica wakati Argentina watakutana uso kwa uso na Ubelgiji. 

Next Post Previous Post
Bukobawadau