Bukobawadau

PITIA TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI JULY 6,2014

Liverpool watafanya jitihada za mwisho kujaribu kumshawishi Ashley Cole kujiunga nao (Mail on Sunday), taarifa nyingine zinasema Cole tayari ameingia mkataba wa miaka mitatu na Roma ya Italy (Sunday People), Everton watatupilia mbali maombi ya Manchester City ya kumtaka Ross Barkley (Liverpool Echo), boss wa Liverpool Brendan Rodgers atamruhusu Martin Skirtel kuondoka iwapo atapata mtu wa kuziba nafasi yake.
Huku Dejan Lovren wa Southampton akitazamwa kuchukua nafasi hiyo (Sunday Express), beki wa Newcastle Matheiu Debuchy amethibitisha kuwa atajiunga na Arsenal msimu ujao (Sunday Express), Newcastle wanatazama uwezekano wa kumchukua beki wa kulia wa Ajax Ricardo van Rhijn kuziba nafasi ya Debuchy (Metro), Liverpool watapewa pauni milioni 75.5 na Barcelona za kumnunua Luis Suarez (Sunday Mirror), kiungo wa zamani wa Chelsea FrankLampard anakaribia ktangaza kujiunga na New York City FC (Daily Star Sunday),
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kumnunua, ama kiungo wa Real Madrid Sami Khedira au Morgan Schneiderlin wa Southampton (Sunday Mirror), Juventus wanataka kulipwa pauni milioni 45 pamoja na Luis Nani ikiwa Manchester United wanamtaka kiungo Arturo Vidal (Daily Star Sunday), Barcelona wamekataa kumsaini beki wa kati wa Liverpool, Daniel Agger, badala yake Barca wanamtaka Mats Hummels (Mundo Deportivo), Juventus wanahaha kumsajili Alexis Sanches lakini watalazimika kuuza wachezaji ili kupata fedha. Juve watakuwa tayaru kuwauza Paul Pogba na Arturo Vidal (Tuttosport), Liverpool huenda wakatumia sehemu ya pauni milioni 70 za Suarez, kumnunua mshambuliaji wa AC Milan Mario Balotelli, ambaye anataka sasa kurejea EPL (Tuttosport).
Newcastle United wanataka kumsajili winga wa Manchester United Wilfried Zaha kwa pauni milioni 7. Zaha alinunuliwa na Man U kwa pauni milioni 15 (Daily Mirror), Manchester United wamekataa ombi la Southampton la kumsajili Javier Hernandez Chicharito (Sunday People). Share tetesi hizi wa wapenda soka.
Next Post Previous Post
Bukobawadau