Bukobawadau

TAARIFA YA KISOMO CHA AROBAINI YA MAREHEMU (BONDIA) IRAKI HUDU (RIP)

 Ndugu wanajumuiya, mabibi na mabwana
Familia ya marehemu (Bondia)  Iraki Hudu,inapenda kuwajulisha maadhimisho ya arobaini ya marehemu Iraq Hudu itayofanyika siku ya 19 Julai 2014 Shughuli hii itafanyika jioni
wakati kufutari nyumbani kwa marehem huko Buguruni ,Rozana,Dar-es-salaam .

Shughuli hii ya arobaini kwa kuwa imengia katika mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhan,familia ya marehem imeamua kutimiza shughuli hii kwa kufuturisha na kisomo.
Kwa heshima na taazima tunawaomba ndugu na jamaaa wote kushiriki katika shughuli hii. Marehemu Iraq, alitutoka tarehe 13.Juni 2014na kuzikwa siku ya 14.Juni 2014 Hivyo hatunabudi kutekeleza wito huu wa kuadhimisha siku ya kisomo chake. Kwa maelezo na habari zaidi, unaweza kuwasiliana na ndugu (Mtoto) wa marehemu kupitia simu hii 0717795070  kwa wanaopiga kutoka nje ya nchi +255 717795070
Asanteni sana.
Pichani Marehemu Bondia  mkongwe Iraki Hudu enzi ya uhai wake kiwapa mafunzo vijana wa klabu ya ngumi ya Ashanti,Ilala Dar es salaam
Wenu, mwakilishi wa familia ya marehemu  Dani Huddu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau