Bukobawadau

FULL-TIME:BRAZIL 1-7 GERMANY # TUNAPATA REKODI MPYA YA KOMBE LA DUNIA #MPAKA HALF-TIME BRAZIL 0-5 GERMANY

 Ni  hali ya hatari, ni haibu kubwa kwa Brazil Vilio vya mashabki vinasika uwanjani  mpaka mapumziko Germany 5-0 Brazil,tunachoweza kukujuza  ni kwamba historia ya nusu fainali ya kombe la dunia kufikia mapumziko ni mabao 3 lakini usiku wa leo tunashuhudia historia mpya 
Kipa wa Brazil  Julio Cesar na Mchezaji  David Luiz wakiwa wameshikilia Jezi ya mchezaji Neymar wakati wakuimba wimbo wa Taifa 
 Shuti kali la Thomas Muller linamfanya kiwa wa Brazil Cesar pichani (kulia) asione wapi mpila umepitia  ni dakika ya 11 Brazil 0-1 GERMANY
  Mchakato wa goli la kwanza kwa Ujerumani lililofungwa na Mchezaji  Thomas Muller pichani (katikati)
 Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia bao la kwanza.
 Ujerumani Miroslav Klose anavunja rekodi ya Kombe la Dunia anapata bao lake la 16
Uwakika wa kucheza fainali Miroslav Klose wa Ujerumani akishangilia bao lake la pili
Anaonekana mchezaji wa  Brazil David Luiz (kushoto) akimtembezea kiwiko mchezaji  Miroslav Klose wa Ujerumani
Muller na Klose wakipongezana. 
 Klose anapiga shuti na kumuacha Mchezaji wa Brazil Fernandinho akito macho
 Bao la ufunguzi la Thomas Muller kuelekea njia ya ushindi wa 7-1
Klose anashangilia baada ya kufunga bao la pili na kuvunja rekodi ya Mkongwe Ronaldo 
Sammy Khedira anaipatia Ujerumani bao la tano ndani ya dakika 29 za kipindi cha kwanza 5-0
 Kwa mchakamchaka Ujerumani  wanavunja rekodi, wanapata magoli 4 ndani ya dakika sita.
Furaha ikitawala kwa mashabiki wa Ujerumani mwanzoni mwa kipindi cha kwanza.
 Miroslav Klose anakuwa mfungaji bora katika historia yaKombe la Dunia historia 
Ilikuwa tabu kidogo pale Beki wa Ujerumani Jerome Boateng alipotaka kumtunishia Marcelo 
 Mchezaji Kroos  anaonekana katika  'Myesipanko' baada ya kufunga bao lake la pili, dakika mbili tu baada ya bao  la kwanza.
Kwa uchungu wanaonekana mashabiki wa Brazili, Ni kama ndoto kwao kuona timu yao inavyo sulubiwa
 Toni Kroos  anatikisa nyavu ikiwa ni bao la 3 kwa Ujerumani
Hakuna njia yoyote wala miujiza ndivyo wanavyo onekana Oscar na Fred wakiwa wamesima katia duara. 
 David Luiz anaweweseka uwanjani kufuatia changamoto dhidi  ya Miroslav Klose 
Kipa Julio Cesar anaangalia tu mpira ukielekea Nyavuni
  Fernandinho, Maicon na David Luiz wakishauliana baada ya Ujerumani kupata bao la 5.
Kiungo wa ujerumani Sami Khedira  akikabiliana na mshambuliaji  wa Brazil Luis Gustavo .
Mlinzi wa Ujerumani  Mats Hummels (chini)anamzuia mshambuliaji Fred pia Oscar anaondoka na mpira 
Huku Furaha kule Majonzi:Wachezaji wa Ujerumani waishangilia waati wachezaji wa Brazil wanaonyesha kukata tamaa ufuatia dhahama inayo wapata usiku wa leo ndani ya Uwanja wa Estadio Mineirao 
Kituko wachezaji 8 wa Brazil wakiwa wamesimama ndani ya bosi  na kumuacha Muller kirahisi  rahisi.
 Mchezaji Toni Kroos (kulia) akishangilia na wenzake
Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer akiwa chini baada ya kuokoa shambulio la mchezaji  Oscar wa Brazil
Bao la 6 la Ujerumani  limefungwa Mchezaji Andre Schurrle mshambuliaji wa timu ya Chelsea 6-0 
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa katia nusu fainali ya kumbe la dunia 2014
Chululu si ndondondo Kidogo Oscar anapata bao la kufutia machozi dakika za mwisho wa mchezo
 Schurrle akitabasamu  baada ya kufunga bao la 7 dakika kumi na moja kabla ya kipenga cha mwisho 
Baada ya Ronaldo sasa Miroslav Klose  ndiye mfungaji bora katika historia ya Kombe la Dunia historia 
 Brazil wameendelea kuvunja rekodi yao ya 94 iliyopita ambapo walifungwa na Uruguay 6-0 ikiwa ni mwaka 1920 katika mashindano ya Copa Amerika
Seven up: Ni mchezaji Andre Schurrle akishangilia goli  la 7 kwa timu ya Ujerumani 
Mchezaji Oscar anaipatia Brazil bao moja la kufutia machozi,Brazil 1-7 Germany
Ishakuwa nongwa Mzee, Ndivyo anavyo onekana Thiago Silva akimtuliza Beki wa Timu yake David Luiz mara baada ya kipenga cha mwisho
FULL-TIME: Brazil 1-7 Germany... no Neymar, no Silva, no hope?
Kwa Nyepesinyepesi  zaidi Unaweza kuni- follow Instagram @mcbaraka
Next Post Previous Post
Bukobawadau