KIKAO MAALUM CHA KAMATI YA TAIFA YA MAAFA (TANDREC) CHAFANYIKA LEO, JIJINI DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Kamati
ya Taifa ya Maafa (TANDREC), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens
Turuka akiongoza Kikao Maalum cha Kamati ya Taifa ya Maafa(TANDREC) ambayo,
inaundwa na Washiriki wakuu katika kukabili Maafa, Kikao kimefanyika leo katika
ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi
Dharura na Maafa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Elias Kwesi, akiwaeleza
wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC) jinsi walivyojidhatiti kuzuia
na kukabili ugonjwa wa Ebola hapa nchini
ambapo alibainisha kuwa hakuna maabukizi
ya ugonjwa huo hapa nchini hadi sasa, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka, Kikao kimefanyika leo katika
ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Taifa ya Maafa (TANDREC) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka
(watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo
mara baada ya kumaliza kikao hicho leo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya
Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.