Bukobawadau

MAHAFALI YA 4 YA DARASA LA SABA SHULE YA KARUME DAY AND BOARDING ENGLISH MEDIUM 2014

 Mgeni Rasmi katika sherehe hizi za Mahafali ya Darasa la Saba, Mh. Fabian Massawe Mkuu wa Mkoa wa Kagera akilakiwa na Mkuu wa Shule ya Karume Day and Boarding English Medium Primary School,Ndugu Self Mkude mara tu alipowasili shuleni hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiwapungia watu mkono mara baada ya kuwasili katika Mahafali ya Darasa la Saba shule ya Shule ya Karume Day and Boarding English Medium Primary School
 Mwalimu wa taaluma akitoa taarifa  ya ufanisi wa kazi yake kwa Mh. Mgeni Rasmi Rasmi na wazazi waalikwa.
Karume shule ya Msingi imeonesha mafanikio makubwa ya Kitaaluma kutokana na ukweli kwamba wameweza kufanya vizuri sana katika mitihani mbalimbalimbali katika ngazi ya taifa, mkoa, Manispaa pamoja na ile ya ndani ya shule.
 MAFANIKIO;Mitihani ya Taifa darasa la nne Karume shule ya Msingi imekuwa katika nafasi ya kwanza  Manispaa kwa Miaka mitano mfululizo ambayo ni 2008,2009,210,2011 na 2012.
 Kwa mwaka Jana 2013 Karume shule ya Msingi ilikuwa ya pili Manispaa Bukoba,ikiwa ni pamoja na kupata wanafunzi wa kuingia katika  nafasi ya kumi bora wavulana na Wasichana.
 Wakati tukiendelea na taarifa hii tunapokea Salaam za pongezi kwa Mr. Mkude ,kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha Ualimu ERA Bi Paschazia Barongo 
Bi Paschazia anasema;'Super Mkude. you deserve to be proud of your hard work. be your future efforts be equally successful and rewarding
 Wanafunzi wa Darasa la Saba wamekuwa wakifanya Vizuri shuleni hapa kila mwaka.
Muendelezo wa matukio mbalimbali Wanafunzi  na wageni waalikwa wakipata huduma ya Chakula.
Taarifa ya Taaluma inaonyesha  Mitihani ya Darasa la Saba  kwa Mwaka 2011 Karume imekuwa ya Kwanza Manispaa kati ya Shule 34, Ikawa ya 1 Kimkoa kati ya Shule 984 ,kwa mwaka huo huo  ikawa ya Sita ( 6) Kitaifa kati ya Shule 15050
Mwaka 2012 Karume imekuwa ya kwanza (1)Manispaa kati ya  shule 35, ya kwanza Mkoa kati ya Shule 984 pia ikawa ya Nne (4)Kitaifa  kati ya Shule16331.(hakika Mr Mkude anastahili pongezi)
Mitihani ya Darasa la Saba;Mwaka  2013 Karume imechukua nafasi ya pili (2)Manispaa kati ya Shule 35, ya nne (4) Mkoa kati ya Shule 903 na ya kumi na tatu (13) Kitaifa kati ya shule 15656.
Mafanikio Makubwa kwa mwaka huu 2014 Tarehe 28-29 Mei 2014 Mitihami ya MOCK  Mkoa , Shule ya Karume imekuwa ya pili (2).PIA mwezi jana tarehe 6-7 AUG 2014 Mock Manispaa Karume imekuwa ya kwanza (1) kati ya Shule 35.
Kupitia Bukobawadau Blog, unaendelea kupata  matukio ya picha katika mahafali ya  nne  ya darasa la Saba 2014 Shule ya Msingi Karume iliyopo maeneo ya Chabitembe Manispaa ya Bukoba.
Kutoka Mkoani Geita pichani Mmoja wa Waalikwa ambaye ni Mkuu wa Shule rafiki na Karume .
Kutokana na mafanikio yaliyotajwa hapo  juu, Karume Shule ya Msingi imepata tuzo ya ngao ya Ushindi  mzuri kitaaluma kutoka ofisi ya Elimu Bukoba Manispaa.
Pia Shule ya Msingi Karume imepata cheti cha kuitambua kuwa miongoni mwa Shule bora Tanzania zinazofanya Vizuri kitaaluma kilichosainiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo  ya Ufundi Mh . Dr.Shukuru J. Kawambwa.
 Katika furaha wanaonekata Wahitimu wa darasa la Saba Mwaka 2014 Karume Shule ya Msingi
Kwa Ishara nzuri ya Matokeo  kama ilivyobainishwa hapo juu, Uongozi wa Shule ya Karume wanayo matumaini makubwa ya kupata Matokeo mazuri zaidi kwenye Mtihani wa Taifa uliofanyika tarehe 10-11 Sep, 2014
Mdau Mmoja wa Waalikwa pichani
Pichani Mdau Chichi Salum, mmoja wa Waalikwa.
 Sehemu ya Walimu wa Shule ya Karume Day and Boarding English Medium Primary School
 Mrs Mkude pichani kulia Kaimu mkuu wa Shule ya Msingi Karume


 Sehemu ya Wazazi wa Wanafunzi pichani
Waalikwa pichani wakiendelea kufuatilia kinacho katika mahafali hayo.
 Meneja wa shule ya Karume English Medium Primary School,pichani Bi Shamila Mkude
Mshereheshaji mahiri Mc Jerry pichani
 Ulinzi dhabiti kuzunguka maeneo ya shule hii.
Karume Day and Boarding English Medium Primary School ,shule hii ilianzishwa  Jan 2005 ikiwa na darasa la chekechea tu.
Walimu wa Kizungu na Wanafunzi wa  shule ya wasichana ya Josiah Girls High School ya mjini hapa ni sehemu ya waalikwa katika mahafali hayo
 Sehemu ya Wanafunzi wa  shule ya wasichana ya Josiah Girls High School
 Bi Jesca Mzazi wa mwanafunzi anayesoma katika shule hii ya wa Shule Karume Day and Boarding English Medium Primary School
  Mdau GSmart Mzazi wa Mwanafuzi shuleni hapo
 Sehemu ya Wazazi wa Wanafunzi waliopo katika shule ya Karume Day and Boarding English Medium Primary School
 Wanafunzi wanao hitimu darasa la saba Shuleni hapa.
 Wanafunzi wa darasa la tatu wakitoa burudani katika kuwaaga Wenzao wanao hitimu hii leo
 Kwa mbali anaonekana Mwanadada Angel.
 Taswira  Viwanja vya Shule ya Karume English Medium Primary School
Mmoja wa Wazazi wa Wanafunzi  shuleni hapo.
Ndivyo mambo yalivyo katika Mahafali ya Shule ya Msingi Karume  pia inafundisha Somo la dini Na kutokana na  umuhimu wa Somo hilo Shule imekuwa ikifuatilia na kuhakikisha wanafunzi wote  wanaabudu  kutokana na imani zao na somo hili limetengewa siku mbili  za J.nne  na Ijumaa kufundishwa katika ratiba kuu ya shule.
 Ukodak ukichukua kasi...
 Mama Mkude pichani kushoto ambaye ni Kaimu Mkurugenzi katika picha na Mwanae Bi Shamila Mkude ambaye ni  Meneja wa shule ya Karume English Medium Primary School

 Burudani ya Ngonjela.
 Yupo pia Ndugu Bashir Kabyemela maarufu kwa jina la (Badae)
 Bi Maua Ramadhan wa Daftari akishiriki katika mahafali haya kama mzazi
Wanachama na Wadau wa Bukoba Veterans ni Sehemu ya waalikwa.
 Wakurugenzi katika picha na Wanafunzi wanao hitimu Darasa la Saba '2014' shuleni hapo.
 Mkurugenzi Katika picha ya pamoja na wanafunzi wahitimu wa Kiume  darasa la saba mwaka 2014


Wahitimu wa kike katika picha na Mkurugenzi wa Shule Ndugu Self Mkude
Mgeni Rasmi na Viongozi wa Bodi ya Shule wakiwa tayari kukabidhi vyeti kwa wahitimu.
 Mgeni Rasmi akikabidhi vyeti vya Wahitimu.
 MATUKIO ZAIDI YA PICHA 250 YANAPATIKA KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK,JIUNGE NASI HIVI SASA KWA KUGONGA MANENO HAYA>> PICHA MBALIMBALI MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI KARUME
 Katika picha ya kumbukumbu.
 Uongozi wa Shule ya Karume umekuwa na Utaratibu wa kuwa na ziara za kielimu ambapo utaratibu huu humjenga mwanafunzi kimazingira na hupata kujifunza mambo mengi.
 Kwa mwaka huu Mwezi Aprili Wanafunzi walitembelea Mbuga ya Wanyama ya Serengeti Walijifunza mambo memgi sana ya Kijiografia, historia na ekolojia ya Wanyama  na pia  kukuza sera ya Serikali ya kudumisha utalii wa ndani
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiendelea kukabidhi vyeti.
 Mara baada ya kukabidhiwa Cheti chake
 Karume na Maendeleo hiyo ni kauli mbiu mpya kutoka kwa Mh. Fabian Massawe
Wahitimu Wakiwa na Vyeti vyao Mkononi
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiongea katika mahafali hayo.
 Ndugu Hamza Ngemera,sehemu ya Waalikwa
 Usisite kutazama Sehemu ya Video ni  bonge la Show kutoka kwa wahitimu hapa Chini,pia tutakuwa na Video ya pili Risala ya Mkuu wa Shule

Kipande cha Video hii ni Burudani kutoka kwa Wahitimu Darasa la Saba Shule ya Msingi Karume
 Ni fursa ya kupata burudani
 Burudani za hapa na pale zikiendelea.
 Katika kuonyesha vipaji, mmoja wa wahitimu akicheza na mpira mgongoni na kuvua tisheti pasipo mpira kudondoka.
 Hakika kijana huyo alitoa mpya, hapo tayari kesha vua tisheti.!
 Zoezi likiendelea  hivyo hivyo kisha anaivaa nguo yake.
 Kijana Rafik Haruna Goronga akifuatilia kile kinacho endelea.
Mpya nyingine namna mtu anavyoweza kujifanya mlemavu wa miguu .
Ule usemi wa wahenga kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni,Huyu ni omba omba anayeigiza kuwa mlemavu wa Miguu.
 Wanafunzi wakiendelea kutoka burudani ya onyesho la sarakasi
Kimichezo Karume wamejipanga vyema pia.
 Kikundi cha Wahitimu wakionyesha  umahiri wao katika Sarakasi
Ngoma ya Kihaya ikilindima...ni mwendo wa 'Akatamba'na  Chenkula... !
Burudani ya Ngoma.
Pichani  anaonekana Mzee Katemana ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Shule ya Msingi Karume ,Mh.Mkuu wa Mkoa Fabian Massawe,walimu wa Shule na Mkurugenzi Super Self Mkude wakicheza ngoma kwa pamoja.
 MC Jerry katika hili na lile.
 Binti Rali Abdugadi akishow love mbele ya Camera yetu
 Furaha kubwa kwa muhitimu pichani mara baada ya kukabidhiwa cheti chake
 Mchungaji Mshana wa Kanisa la EFATHA akitoa Sala.
 Sala ya Chakula kutoka kwa Kateksta Costatine wa Shule ya Msingi Karume.
 Anaonekano Mmoja wa Waalikwa pichani

SEHEMU YA PILI YA VIDEO RISALA KWA MGENI RASMI MWISHO.

MATUKIO ZAIDI YA PICHA 250 YANAPATIKA KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK,JIUNGE NASI HIVI SASA KWA KUGONGA MANENO HAYA>> PICHA MBALIMBALI MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI KARUME

Next Post Previous Post
Bukobawadau