Bukobawadau

HIJA KWA BIKIRA MARIA NYAKIJOGA-LURDI YA BUKOBA OCT 19, 2014

 Baba Askofu Methodius Kilaini akitoa baraka wakati wa misa ya hija-Nyakijoga,Parokia ya Mugana
 Baadhi ya Wakatoliki wakishiriki Ibada ya misa ya hija
 Bw Prosper Mbakile akisoma risala kutoka Parokia ya Bukoba
Baadhi ya watawa-masista,na mapadre katika misa hiyo ya hija
 Pichani anaonekana Mwanamama kutoka Parokia ya Katoma akisoma Risala
 Misururu ya Waamini wanaosubiri zamu za kuchota maji ya baraka
Umati mkubwa wa Waumini 
 Kanisa la Bikira Maria,Nyakijoga
 Baadhi ya watawa-masista,na mapadre katika misa hiyo ya hija
 NA MUTAYOBA ARBOGAST,NYAKIJOGA-MUGANA
MAELFU  ya Wakatoliki na waamini wengine 19-10-2014 wamekusanyika katika eneo eneo la Nyakijoga,Parokia ya Mugana,Jimbo Katoliki la Bukoba kwa ajili ya hija.

Waamini hufika Nyakijoga kila mwaka kwa maombezi ya Bikira Maria,Mkingiwa wa dhambi yaasili  Eneo hilila Nyakijoga lina pango linaloshabihiana na pangola Lurdi nchini Ufaransa ambako Bikira Mariaalimtokea mtoto Bernadetta Subiru mwaka 1858.

Eneo hili linalobubujika maji yanayoaminika kuwa na baraka na kuponya magonjwa mbalimbali,

Iilitangazwa na mwaka 1958  na Baba Mtakatifu kuwa wanaohiji Nyakijoga wana thawabu sawa na wale wanaohiji Lurdi.
 Parokia mbalimbali na taasisi za dini kutoka ndani na nje ya Jimbo Katoliki la Bukoba,licha ya kuombea wanadamu kuishi na kutenda kadri ya mapenzi ya mungu,zimetaka maridhiano ya kupata katiba mpya yaendelee kushughulikiwa na serikali,ili jambo hilo lisiharibu amani
ya nchi yetu.

Askofu Methodius Kilaini ambaye ni Askofu msaidizi wa Jimbo, ambaye ameendesha ibada ya misa takatifu,amewataka wananchi kusoma vizuri ‘katiba pendekezwa’ na kuipigia kura kadri ya utashi wa mtu mwenyewe bila kurubuniwa wala kununuliwa.

Alihudhuria pia Askofu mstaafu Nestori Timanywa,huku Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba,

Desderius Rwoma hakuweza kuhudhuria kutokana na udhuru

Next Post Previous Post
Bukobawadau