Bukobawadau

VIDEO/PICHA YALIYOJIRI KATIKA HARAMBEE YA UCHANGIAJI UJENZI WA MAABARA MASHULENI MANISPAA BUKOBA OCT 30,2014

Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa (Mb),mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Uhuru  Mjini hapa katika shughuli ya harambee ya halmashauri ya Manispaa Bukoba kwa ajili ya Ukusanyaji  wa michango ya  Ujenzi wa Maabara Mashuleni 
 Ufunguzi wa Shughuli ya Harambee ya michango ya Maabara ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba iliyofanyika katika Viwanja vya Mayunga 0ct 30,2014.
 Mgeni Rasmi Mhe. Kassim Majaliwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akiwahutubia wananchi waliojitokeza  katika  Harambee ya ujenzi wa maabara katika  shule za  sekondari kama  ikiwa ni  sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dr Kikwete .
 Katika kile kinachoonyesha ni kuunga mkono maagizo ya Rais Dr Jakaya Kikwete katika uanzishaji ujenzi wa maabara za sayansi katika shule za sekondari Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd Ndg James Lugemalira ametoa  Mchango wa mifuko 500 ya Cement.
 Msemaji wa Kampuni ya Kampuni ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd Ndg Andrew Kagya aki
Akizungumza katika harambee ya  kuchangia  ujenzi  wa maabara  katika shule za Halmashauri ya Manispaa Bukoba.

 Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa akipitia hati ya shukrani kwa kabla ya kumkabidhi Mwakilishi wa Kampuni ya Kampuni ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd
Kwa kutambua umuhimu wa kuchangia maendelea Ndg Rahym Kabyemela anapokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mh.Naibu Waziri Mhe. Kassim Majaliwa.
 Pichani kushoto ni msemaji wa Kampuni ya Mabibi Beer tawi la Bukoba Ndg Andrew Kagya.
 Naye  Mbunge wa Bukoba Mjini na Mdau wa maendeleo katika  jimbo lake Balozi Hamisi Kagasheki katika kuungwa mkono maagizo ya  Rais Mheshimiwa Dr  Jakaya mrisho  Kikweteameahidi kutoa milioni 30.

Katika kile kinachoonyesha ni kuunga mkono maagizo ya Rais Dr Jakaya Kikwete katika uanzishaji ujenzi wa maabara za sayansi katika shule za sekondari Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd Ndg James Lugemalira ametoa  Mchango wa mifuko 500 ya Cement. 

 Naye Mchungaji King James ametoa Mifuko 150 ya Cement yenye thamani ya shilingi milioni tatu na katika hali ya kuendeleza ushirikiano Kamanda wa Vijana wa CCM wa Kata ya Bilele Ndugu Ashraf Kalumuna amechangia bando 5 za mabati ambazo zina thamani ya Tsh 1,250,000 ,makundi mengine yameweza kutoa mchango huo wa hiari ambapo watumishi wa Manispaa na Wakuu wa Idara wamekabidhi jumla ya mil.8,501,900

 Wakati Mama Tibaijuka kupitia shule ya Kajumulo amekabidhi mchango wake kiasi cha shilingi million 1,pia Mama Mshashu MBUNGE amechangia kiasi cha million 1.
Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda katika hili wametoa mchango wao shilingi laki moja 

Mjumbe wa NEC CCM wa wilaya ya Bukoba Mjini , Ndugu Abdul Kagasheki amechangia kiasi cha shilingi laki tano.Wakati unaendelea kupitia matukio haya katika picha 200 tunakukumbusha kuwa Zoezi hili bado linaendelea.
Sehemu ya Wadau wa Elimu waliojitokeza katika harambee ya kuchangia Ujenzi wa Maabara
 Kushoto ni Mchungaji King James wa kanisa la ukombozi manispaa ya Bukoba
 Mchungaji King James akiongea wakati wa  kushiriki harambee ya kuchangia  ujenzi wa maabara za  sayansi mashuleni ambapo ametoa Mifuko 150 ya Cement yenye thamani ya shilingi milioni tatu.
Taswira Viwanja vya Uhuru (Mayunga)
  Kamanda wa Vijana wa CCM wa Kata ya Bilele Ndugu Ashraf Kalumuna akikabidhiwa nishani ya shukrani kufuatia mchango wake wa  bando 5 za mabati ambazo zina thamani ya Tsh 1,250,000.


 Meneja wa Bank ya CRDB tawa la Bukoba
Muendelezo wa Matukio kutoka Viwanja vya Uhuru (Mayunga ) Mjini Bukoba
 Wadau wakiendelea kufuatilia kinachojirikatika Viwanja vya Uhuru(Mayunga0
Wanahabari wakiwajibika
 Mc Jerry mwendeshaji wa Shughuli hii akiwajibika.
Mnenguaji wa Saida Karoli akifanya yake katika Wimbo Maria Salomela
Burudani kutoka kwa Msanii Saida Karoli, mwana mama mwimbaji anayevuma kwa sasa na nyimbo yake ya 'Akatambala'
Hivi ndivyo Wadau mbalimbali walivyoweza kuitikia Zoezi la Uchangiaji wa Maabara mashuleni.
 Ndugu Jamal Kalumuna akiongea Jambo kwa niaba ya Mdogo wake Ndg Ashraf
 Ndg Felix Flancis Mulokozi mwakilishi wa shule ya Sekondari ya Wasichana 'Kajumulo Girls High School' mara baada ya kukabidhi mchango wao kiasi cha shilingi Milioni moja
 Mtoto Mdogo akitoa Mchango wake
Kwa niaba ya Al Amini Abdul kiasi cha Shilingi laki Moja kinakabidhiwa na Mc Jerry kwa
 Anaonekana Mwanadada Jane ambaye ni Mc No. 2 katika Shughuli hii.
 Waakilishi wa chama cha Waendesha pikipiki maarufu kama Assecdo
 Mr Mwamsonjo akipongezwa na Mh.Naibu Waziri Kassim Majaliwa mara baada ya kutoa Mchango wake


Chondechonde jamani!!...Kupitia picha hii tunawaomba wadau wengine 'Nshomile' waliopo Ndani na nje ya Manispaa ya Bukoba kuunga mkono  jitihada hizi ili kufanikisha  Ujenzi wa ujenzi wa maabara mashuleni.
Saida Karoli katika Mahojiano na mwanahabari
Katika pozi ni Mnenguaji wa Saida Karoli
Usisite kupitia sehemu ya Video mwisho wa ukurasa huu upate kuona Vionjo vya Msanii Nshomile mwenye kipaji cha aina yake ,na mtunzi mzuri sana wa mashairi na mwenye mshabiki wengi sana akifanya yake kwa LUGHA ya Asili katika kuamasicha Uchangiaji wa Maabara Mashuleni
 Mwakilishi wa Shirika la Umeme Tanesco.
 Mr. Shafih kwa niaba ya Mh Abdul Kagasheki (Kananga)Mjumbe wa NEC CCM wa wilaya ya Bukoba Mjini ,aliyeweza kuchangia kiasi cha Shilingi laki tano.


 Dr.Baruti  akiongea mbele ya Mh. Naibu Waziri mara baada ya kutoa mchango wake
 Wakuu wa Shule za Msingi Manispaa ya Bukoba wakiwakirisha kile walichonacho .
 Kutoka Manispaa ya Mji Bukoba  michango ya Watumishi ikikabidhiwa  kutokana na Idara husika.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa akiendelea kusimamia zoezi la harambee hiyo.
 PITIA SEHEMU YA VIDEO YALIYOJIRI KATIKA UTARATIBU WA UCHANGIAJI WA  MAABARA SHULE ZA SEKONDARI BUKOBA KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA INGIA HAPA>>Bukobawadau Entertainment Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau